Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 49 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 640 2023-06-15

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mulungu Jimbo la Muhambwe?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedha wa 2023/2024 Serikali imetenga bajeti ya shilingi milioni 500 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kizazi. Aidha wananchi wa Kata ya Kizazi wamejenga jengo la OPD hadi kufikia hatua ya lenta.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya kwenye Kata za kimkakati kote nchini ikiwemo Kituo cha Afya katika Kata ya Mulungu.