Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 56 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 734 2023-06-27

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Primary Question

MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kupandisha hadhi Mji wa Magugu?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, uanzishaji wa Mamlaka za Miji Midogo hufanyika kwa kuzingatia Sheria ya Mipango Miji Namba 8 ya mwaka 2007 pamoja na Mwongozo wa Uanzishaji wa Maeneo ya Utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wa mwaka 2014 ambapo umeanishwa utaratibu na vigezo vinavyopaswa kufuatwa.

Mheshimiwa Spika, kusudio la kupandisha hadhi Mji wa Magugu lipo katika hatua za upangaji wa Mji ikiwemo uandaaji wa mpango wa jumla na mpango kina ambapo ikikamilika itatangazwa kupitia gazeti la Serikali.