Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 56 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 745 2023-06-27

Name

Ndaisaba George Ruhoro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa soko la mnada wa ng’ombe wa Murusagamba?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa miundombinu ya mnada wa mpakani wa Murusagamba umekamilika na ulihusisha ujenzi wa uzio, mazizi na ukarabati wa ofisi. Baada ya ujenzi kukamilika Wizara inaandaa utaratibu wa kuanza kuhamasisha wafanyabiashara na wafugaji kuanza kutumia mnada huo ili kufanikisha mauzo ya mifugo nje ya nchi na kuongeza maduhuli kwa Serikali Kuu na Halmashauri.