Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 55 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 728 2023-06-26

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaboresha miundombinu ya Chuo cha VETA Kitangari?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuongeza baadhi ya majengo yanayokosekana katika Chuo cha VETA cha Kitangari ili kuimarisha uwezo na ufanisi katika kutoa mafunzo yaliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetenga fedha kiasi cha shilingi 666,904,745.01 kwa ajili ya kukiimarisha Chuo cha VETA Kitangari ikiwemo ujenzi wa mabweni, jiko, bwalo la chakula, madarasa na nyumba za watumishi. Ujenzi wa majengo hayo umeanza mwezi Mei, 2023, ahsante.