Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 54 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 704 2023-06-23

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati zahanati 18 katika Tarafa za Laela, Mpui, Mtowisa na Kipeta?

Name

Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, inaendelea kufanya tathmini ya majengo yote chakavu yanayohitaji ukarabati ili yaweze kukarabatiwa na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa zahanati kongwe kote nchini zikiwemo zahanati 18 katika Tarafa za Laela, Mpui, Mtowisa na Kipeta katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.