Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 53 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 701 2023-06-22

Name

Ameir Abdalla Ameir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR aliuliza: -

Je, kwa kiwango gani TEHAMA inatumika kuboresha sekta ya kilimo nchini?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ameir Abdalla Ameir, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Kilimo ni mojawapo ya sekta zinazonufaika na maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini. Kwa kutumia TEHAMA sekta ya kilimo imeboresha maeneo mbalimbali ya huduma zinazotolewa na Wizara kwa wakulima, wafanyabiashara na wadau mbalimbali katika sekta na umma kwa ujumla. Baadhi ya huduma zilizoboreshwa kwa kutumia TEHAMA ni pamoja na kutoa huduma za ugani kwa wakulima, masoko ya mazao ya wakulima, kutoa mbolea ya ruzuku, kupata vibali ama leseni za kufanya biashara za mazao ya mimea na vyeti vya afya ya mimea kwa mazao yanayosafirishwa nje ya nchi.