Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 251 2022-05-24

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itafungua Zahanati iliyopo Kijiji cha Nyakashengi Kata ya Businde ili iweze kutoa huduma kwa wananchi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate, Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Zahanati iliyopo kwenye Kijiji cha Nyakashengi, Kata ya Businde tayari imeshasajiliwa kwa usajili Na. 120780-2 kutoka Wizara ya Afya na kuanza kutoa huduma tangu tarehe 15/04/2022. (Makofi)