Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 29 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 257 2022-05-24

Name

Aleksia Asia Kamguna

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha kilimo cha Mpunga katika Mkoa wa Morogoro?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aleksia Asia Kamguna, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imetekeleza mradi wa Kuongeza uzalishaji na tija ya zao la Mpunga katika Mkoa wa Morogoro. Matokeo hayo yamechagizwa na kuongezeka kwa upatikanaji wa mbegu bora za mpunga.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mpunga ulifanyika katika Halmashauri za Wilaya za Mlimba, Ifakara, Kilosa na Mvomero ambapo jumla ya maghala matano yamejengwa.