Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 31 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 268 2022-05-26

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Watumishi wa Kada ya Afya Wilayani Kalambo kwa kuzingatia upungufu uliopo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka huu wa fedha imepanga kuajiri watumishi wa kada ya afya 7,612 watakaopangiwa katika Halmashauri zote nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.