Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 31 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 272 2022-05-26

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-

Je, ni lini Mradi wa Umwagiliaji wa Kijiji cha Arusha Chini utatengewa fedha ili uanze kutekelezwa?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Umwagiliaji katika Kijiji cha Arusha Chini una jumla ya hekta 120 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Kati ya hizo hekta 48 zinamwagiliwa kwa kutumia mifereji ya asili ambayo chanzo chake cha maji ni chemichemi na mvua za msimu. Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa skimu hii.