Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza: - Je ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Momba na lini huduma za Mahakama za Mwanzo zitaanza kutolewa katika Tarafa ya Msangano?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Katika Wilaya ya Songwe, ujenzi wa Mahakama umeshaanza tangu mwaka jana, je, lini Serikali itamaliza ujenzi katika Wilaya hii? Hilo ni swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, lakini changamoto za Mahakama katika Wilaya ya Ileje ni nyingi sana katika Tarafa zote mbili Mbundali na Ulambia, sasa nilitamani kufahamu ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha katika tarafa hizi zote kutakuwa na majengo ya Mahakama? Ahsante.

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katibu na Sheria, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, umaliziaji wa jengo la Songwe kimsingi upo mwishoni kabisa, ni matarajio yetu katika muda mfupi ujao jengo lile litaweza kukamilika na kwa sababu lilikuwa kwenye mpango huu unaoishia mwezi wa sita na baada ya kikao hiki cha Bunge tutakwenda kuliangalia ili tujue wapi wamekwamia kwa sababu ilikuwa limalizike haraka.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu Mahakama za Ileje, mpango wa Serikali hadi kufikia mwaka 2025 makao makuu yote ya tarafa nchini tutakuwa tumejenga Mahakama ambazo zitakuwa ni bora na nzuri kabisa. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mwandabila baada ya kikao hiki cha Bunge tuwasiliane ili nimpe detail ya mpango kazi ambao tumeuweka kwenye suala la ujenzi wa Mahakama zetu, ahsante. (Makofi)