Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sebastian Simon Kapufi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Mjini
Primary Question
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI K.n.y. MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itawaajiri vibarua wapatao 20 ambao wamefanya kazi Shirika la Reli Mkoa wa Katavi kwa miaka mitano?
Supplementary Question 1
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru ninalo swali moja dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu spika, naipongeza Serikali kwa majibu yake mazuri na kwa kuwa Serikali imekiri kwamba vijana hawa wamekuwa wakifanya kazi nzuri nafahamu wapo ambao walifanya toka enzi za TRL. Je, Serikali inasema nini katika kuzingatia mafao yao wakati wa kuajiri?
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. FREDY A. MWAKIBETE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Kapufi, Mbunge wa Mpanda Mjini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Serikali nipokee hizo pongezi za Mheshimiwa Mbunge na nipende kujibu swali lake la nyogeza kuhusu namna ambavyo Serikali inazingatia hawa vibarua kwa ajili ya maslahi yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwisha kusema kwenye jibu langu la msingi kwamba Serikali kupitia Waraka Namba Moja wa mwaka 2004 wa Utumishi wa Umma kwamba anayestahiki ama anastahili kuajiriwa katika ajira za kudumu inatakiwa awe amemaliza kidato cha nne, na hawa kwa kuwa wako darasa la saba na wengine hawajamaliza tunaendelea kuwashawishi na kuwashauri na kupitia Shirika letu la Reli nchini tutaendelea pia kuwaendeleza ili wafikie hicho kiwango na hatimaye kuajiri.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved