Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Halima James Mdee

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HALIMA J. MDEE aliuliza: - Je, Serikali inadaiwa fedha kiasi gani ilizokopa Mifuko ya Hifadhi za Jamii na kiasi gani cha madeni kimelipwa na kwa utaratibu gani?

Supplementary Question 1

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, majibu ya Waziri yanaonesha kwamba deni la pre-1999 ni shilingi trilioni 4.4 lakini ripoti ya kikosi kazi cha Serikali yenyewe pamoja na ripoti ya CAG ambayo ilitolewa mwaka 2015 inaonesha deni la Serikali la pre-1999 ni shilingi trilioni 7.1.

Sasa nataka Waziri uniambie hiyo tofauti ilitokea lini na wapi na kwa sababu gani?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili Mfuko wa NSSF umesema Serikali inadaiwa shilingi bilioni 292 ripoti ya CAG iliyotoka juzi inasema Serikali inadaiwa shilingi trilioni 1.17 hiyo tofauti kati ya bilioni 200 na trilioni moja imetokana na nini?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza alikuwa anaulizia tofauti imetokeaje, naomba hili tulichukue kama ni ushauri na tutamjibu kwa njia ya maandishi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili pia amehitaji tofauti tunaomba pia tulichukue na kwenda kufanya review bila shaka tutapata majibu yaliyo sahihi. (Makofi)