Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nancy Hassan Nyalusi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, Serikali inachukua hatua gani za kukabiliana na athari mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na hali ya kisiasa duniani?

Supplementary Question 1

MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwenye tathmini ya Serikali kati ya bidhaa ambazo zimeathiriwa na vita ya Urusi ya Ukraine ni mafuta ya nishati, mbolea na ngano.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kufuta VAT kwa wazalishaji wa mafuta ya kula ndani ya nchi? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala hili limejadiliwa na suala hili ni ushauri, linahitaji wataalam, tutakaa pamoja tutatoa majibu. Nadhani pengine leo ama kesho tutatoa jibu la suala hilo.