Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUNGULILE aliuliza:- Je, ni kiasi gani cha fedha kimekusanywa tangu Daraja la Nyerere lianze kutumika na ni lini huduma ya daraja hili itatolewa bila malipo?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUNGULILE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; nataka kujua kwamba kwa sasa kimebaki kiasi gani cha deni la gharama za ujenzi ambacho kimebaki?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa mujibu wa majibu ambayo amenipa kwamba tarehe 21 Mei, 2022 walifanya mapitio ya tozo za daraja na kuanzisha utaratibu wa tozo za siku, wiki na mwezi. Je, ni lini utaratibu huu wa tozo za siku, wiki na mwezi utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakamilisha mfumo wa kuanza tozo kwa siku, wiki na mwezi; nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunategemea kwamba kuanzia tarehe 1 Julai, 2022, mfumo huu utaanza kutumika. Ahsante.