Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza: - Je, kwa nini wakulima wa kahawa Mbozi wanakatwa shilingi 200 kwa kilo licha ya tamko la kusitisha tozo hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza kabisa, Mheshimiwa Waziri wakati akihitimisha bajeti hapa alisema kwamba hiyo tozo atakuwa analipa mnunuzi, na kwa hiyo wakulima wa arabica nchini hawatalazimika kulipa shilingi 200.

(a) Je, kwa nini bodi bado inaendelea kuwatoza?

(b) Je, kwa nini basi mnunuzi asiambiwe rasmi kwamba awe analipa hiyo, na ijulikane kwenye Hansard?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli Mheshimiwa Waziri alipokuwa anazungumza hapa wakati wa Bunge alilitolea ufafanuzi, na ndiyo maana hii bei ya shilingi 200 ikawa inawekwa katika bei ile ya jumla ya soko, kwa maana mnunuzi analipa moja kwa moja na katika ile sehemu mkulima anakatwa. Hata hivyo, mapendekezo yake sisi tunayapokea na tutayapitia upya ili tuone namna bora ambayo mkulima ataona athari za moja kwa mojo za makato hayo ya shilingi 200. Ahsante sana.