Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Kilumbe Shabani Ng'enda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Mjini
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA K.n.y. MHE. ZAINAB A. KATIMBA aliuliza: - Je, lini Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi itaanza kujengwa?
Supplementary Question 1
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA: Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kwamba Mkoa wa Kigoma uko pembezoni na Hospitali za Rufaa za Kanda zote, ambazo ni za Bungando na Benjamin Mkapa, zipo mbali; Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza kasi kubwa katika kujenga Hospitali hiyo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili; Wakati tukisubiri hospitali hiyo ya Kanda, Je, Serikali haioni umuhimu wa kuimarisha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Maweni, hasa kukamilisha Jengo la Wagonjwa wa Nje OPD?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba yeye ni shahidi kwa kasi kubwa inayofanyika pale. Leo tumekwenda mimi na yeye kwenye Hospitali ya Mkoa, ameona baadhi ya kliniki sasa zinatoa huduma za kitaifa ambazo zilitakiwa zitolewe Muhimbili, lakini zinatolewa pale kwa sababu ya alichokisema Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Spika, pia ameona kiwango ambacho lile Jengo la OPD limefika, nakuhakikishia litakwisha. Na kama ambavyo tumesema hapa Mwezi Januari ujenzi wa Hospitali ya Kanda unaenda kuanza, utaenda kuanza kama tulivyosema hapa na tutahakikisha inaenda kwa kasi kwa kuzingatia uhitaji wa watu wa Kigoma na umbali kutoka kwenye Hospitali za Taifa na zingine za Kanda.
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA K.n.y. MHE. ZAINAB A. KATIMBA aliuliza: - Je, lini Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi itaanza kujengwa?
Supplementary Question 2
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kumuuliza swali la nyongeza Mheshimiwa Waziri;
Je, ni lini Zahanati za Jimbo la Lushoto zitapata vifaa tiba vya kutosha?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge, swali lake zuri. Kama ambavyo alishuhudia wiki mbili zilizopita, Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua vifaa mbalimbali. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge nikienda kukaa kwenye kiti changu, aje hapa tuwasiliane na DM wake aorodheshe vinavyohitajjika, ili tuweze kupeleka mahitaji MSD mara moja, vifaa vianze kupelekwa kwenye Zahanati zake za Lushoto.
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA K.n.y. MHE. ZAINAB A. KATIMBA aliuliza: - Je, lini Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi itaanza kujengwa?
Supplementary Question 3
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Hospitali wa Mkoa wa Simiyu haina uzio kabisa na hospitali ikikosa uzio ni hatari sana;
Je, ni lini Serikali itajenga uzio katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimepokea ombi lake la uhitaji wa uzio; lakini nimuombe Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu kwanza, Hospitali hiyo ya Simiyu ni mpya na iko bado kwenye ujenzi, Tukamalizie kwanza majengo ya kimkakati ambayo bado yanahitajika kujengwa kwenye eneo hili. Tukimaliza tutaelekea kwenye eneo la uzio kama ambavyo yeye Mheshimiwa Mbunge ameshauri, ahsnate sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved