Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: - Je, Serikali haioni umuhimu wa kugawa mizinga ya nyuki ili kubadili shughuli za kiuchumi zinazoharibu mazingira kama kukata miti na mkaa Iringa?

Supplementary Question 1

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, naomba sasa niwe na swali moja tu la nyongeza. Kwa kuwa maelezo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri umeyaeleza, vikundi vingi vilivyopewa mizinga hiyo ni vya Wilaya ya Iringa lakini kutoka Iringa Vijijini na Iringa Manispaa ni lango la utalii Kusini.

Je, mpo tayari sasa kutupatia na Iringa Manispaa ili angalau uoto wa asili urudi kwa kufuga nyuki? Ahsante. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jesca Msambatavangu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mara tutakapopata orodha ya vikundi vilivyoanzishwa kwa jambo hili, Wizara itaona jinsi ambavyo inaweza kushirikiana na hamashauri ili kuweza kuwapatia mizinga. (Makofi)