Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, kwa nini NHIF inazuia matibabu ya baadhi ya wagonjwa wenye Bima za Afya wakiwa hospitali?

Supplementary Question 1

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, naomba nikiri kwamba, jibu la Mheshimiwa Naibu Waziri ni zuri sana. Ni jibu la ukweli na nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la kwanza; kwa kuwa ni kweli kwamba baadhi ya watumishi wamelelewa kama watoto yatima lakini wamelelewa na watu ambao siyo biological fathers au parents na tofauti ya majina ndiyo iliyoleta shida ya kufutiwa hizo NHIF, ni utaratibu upi wa haraka unafanywa ili hao waliofutiwa waweze kupata huduma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, wakati wa zoezi hili wako watu walinyang’anywa kadi hizi wakiwa hospitali na wale watumishi wakapelekwa polisi na kufunguliwa mashtaka. Ni nini kimefanyika Wizara ya Afya, kwanza kuwaachia wale watumishi lakini kufuta mashtaka hayo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili mazuri ya Mheshimiwa Kanyasu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja, anaelezea kwamba kuna watu ambao wamelelewa na wazazi ambao siyo wazazi wao biologically lakini ndiyo walezi wao ambao wamewalea. Kwa sababu sasa ndiyo tumepitisha juzi Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote na tunaenda kutengeneza kanuni na taratibu, mafikiri jambo ambalo amelizungumzia hapa litaenda kuangaliwa kwa kina na kuona ni namna gani linaweza likatatuliwa lisiweze kutokea tena. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia amezungumzia wale ambao wamekutwa wakiwa hospitalini na wamenyang’anywa na wengine wameshtakiwa. Mimi ninachoweza kusema kuna pande mbili. Kuna ambaye amenyang’anywa lakini kweli amelifanya hilo kosa, taratibu za kisheria zitachukua mkondo wake lakini kuna wengine ambao ni makosa mengine ya wataalam wetu kutoa kadi inayotofautiana jina na hali halisi iliyoko kwenye vyeti vyake. Hilo tutaenda kuangalia kwa individual na kuona jinsi ya kutatua. Kwa sababu, pia inawezekana kwenye jimbo lako kuna mambo yaliyotokea kama hayo.

Mheshimiwa Spika, tutaenda kuangalia specifically tuone namna gani tutatatua kwa pamoja na tutumie mfano huo kutatua mengine, kwa maana ya nchi nzima. Ahsante sana. (Makofi)