Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa kutosha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara?

Supplementary Question 1

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwa sababu matarajio ya Hospitali ile ya Rufaa ni kutoa huduma za kibingwa, lakini kwa sasa tuna Daktari Bingwa mmoja tu; na katika jibu la msingi amesema kwamba anasubiri ajira mpya; je, ni lini Serikali italeta Madaktari Bingwa ili huduma za kibingwa zianze kutolewa katika hospitali hiyo?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, ni kwamba, ili wataalam hao waweze kufanya kazi kwa ufanisi, wanahitaji vifaa. Tunashukuru Serikali kwa kutuletea fedha za ununuzi za MRI na CT-Scan, lakini kwa sababu hawana Bodi ya Manunuzi, vifaa hivyo vimeagizwa kupitia Ocean Road; je, ni lini vifaa hivyo vitapatikana katika hospitali yetu ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Abdallah Chikota, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, moja la kwanza kuhusu ma-Specialist, inapofikia mwezi Julai mwaka huu 2022, kwa sababu tayari ma-specialist wawili wako pale na kwenye kibali hiki wako ma-specialist wanane, kwa hiyo, hospitali hiyo itakuwa na ma-specialist 10.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni kuhusu vifaa tiba. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, vifaa hivyo viko kwenye manunuzi, na tayari viko kwa ajili ya kuja nchini mpaka Oktoba vitakuwa vimefungwa na kazi itakuwa imeanza. (Makofi)

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa kutosha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara?

Supplementary Question 2

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Katika mgao wa watumishi wa afya ambao umefanyika juzi, nimeona bado katika vituo vyangu vya afya vya Kasaunga, Kisorya na Kasuguti havikupata; je, nini kauli ya Serikali sasa kuhusiana na upungufu huo?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba aliona Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI akisema kuna nafasi zaidi ya 700 ambazo bado hazijapata watu, lakini kwenye Wizara ya Afya kuna nafasi vilevile ambazo zinaweza zikabaki. Watashirikiana Waziri wa Afya na Waziri wa TAMISEMI kuona, na aje tupange ili tuone ni namna gani inaweza kufanyika ku-fill hizo gap anazozisema. (Makofi)

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa kutosha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara?

Supplementary Question 3

MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi. Nami naomba niulize swali moja.

Mheshimiwa Spika, mahitaji ya watumishi wa afya wanaohitajika katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala ni 624, waliopo mpaka sasa ni 119 sawa na asilimia 19, na tuliopata juzi ni 38 tu, upungufu bado upo; je, Serikali inasema nini kuhusu kujaza nafasi za watumishi katika kada ya afya kwa Halmashauri ya Jimbo la Newala Vijijini? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ninachoweza kumwambia Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, jinsi ambavyo bajeti itaendelea kuruhusu, maeneo kama hayo ambayo anayasema Mheshimiwa Mbunge yataendelea kupewa kipaumbele. Utaona wakati wa application wa hizi nafasi zilizotangazwa, umeona kabisa yameainishwa maeneo ambayo wanaruhusiwa watumishi ku-apply na wametajiwa kabisa utaenda hapa, utaenda hapa. Tutaendelea kusisitiza kabisa maeneo yenye upungufu zaidi yanapotokea kibali ndiyo yapewe kipaumbele. (Makofi)

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa kutosha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara?

Supplementary Question 4

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Jimbo la Tabora Mjini lina Hospitali ya Rufaa ya Kitete. Hospitali hii ina upungufu wa Madaktari Bingwa wasiopungua tisa na ni ahadi ya muda mrefu Serikali kutuongezea Madaktari Bingwa. Sijui Serikali itatuletea lini hao Madaktari Bingwa? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna shida ya Madaktari bingwa; japo wapo, lakini hawatoshi. Niendelee kumwomba Mheshimiwa Mbunge tushirikiane mimi na yeye kwa sababu kuna ambao wako shuleni sasa hivi, tena wengine wanatokea pale Kitete. Vile vile jinsi ambavyo wanamaliza tuendelee kuwapangia na kwa sababu sijaiangalia Kitete specifically, tutaangalia kwenye mgao huu kama kuna kilichofanyika kwenye eneo la Kitete.

Name

Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa kutosha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara?

Supplementary Question 5

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Ni lini Serikali itaongeza wafanyakazi kwa maana ya Matabibu katika Kituo cha Afya cha Matemanga, Nakapanya na Mtakanini?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, maeneo aliyotaja Mheshimiwa Mbunge ni mojawapo ya maeneo ambayo hata sisi tunajua yana watumishi wachache na ni maeneo ambayo wengi wakipangiwa wanahama. Namwomba Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo nilimjibu Mheshimiwa Mbunge mwenzake, kwenye nafasi ambazo ametangaza Waziri wa TAMISEMI ametaja, tukutane tuangalie na sisi upande wa Afya tuweze kuona namna ya kutoa kipaumbele kwa maeneo hayo kwenye hizi nafasi ambazo zilipungua.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa kutosha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara?

Supplementary Question 6

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Mji wa Bunda ina mahitaji ya watumishi wa afya wakiwepo Madaktari na Manesi 402. Waliopo ni 184, mahitaji ni 218: Je, katika hizo ajira mpya katika mgao wa nchi nzima, Halmashauri ya Mji wa Bunda ni sehemu mojawapo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naweza kumwambia ni sehemu mojawapo ambayo inafikiriwa kupangiwa, lakini wala asiogope kwa sababu inapokwenda kuwa Hospitali ya Nyerere, ile ya Kanda ambayo inajengwa Mara nayo ni sehemu mojawapo ambayo itakwenda kupunguza mahitaji ya watumishi kwenye eneo hilo la mkoa wao.

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka Watumishi wa kutosha katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara?

Supplementary Question 7

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa napenda kuishukuru Serikali kwa kutuletea vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Rukwa; je, ni lini sasa Serikali itatuletea Daktari Bingwa wa mifupa? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nadhani swali la Mheshimiwa Mbunge ni specific. Naomba tuje tuangalie kama eneo, kuona kama Mkoa huo hauna kabisa Daktari wa mifupa, tukae na Mheshimiwa ili tuhakikishe kabla ya mwezi wa Oktoba amepatikana. (Makofi)