Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza:- Je, ni lini ombi la kubadilishana Hospitali ya Mkoa na ya Wilaya litafanyiwa kazi kuruhusu upanuzi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa?
Supplementary Question 1
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza naishukuru Serikali kwa majibu mazuri ambayo wametupatia, nami nakubaliana nayo na wala hatuna shida kwenye majibu hayo, isipokuwa tu, tutakapokuja kujadiliana nafikiri tunaweza tukafikia muafaka.
Mheshimiwa Spika, kwanza tunawashukuru kwa watumishi mliotuletea 26 ndani ya Manispaa ya Iringa wanaokwenda kwenye zahanati zetu na vituo vya afya na kwa ajili ya ujenzi wa wodi pale Frelimo. Ili kupunguza changamoto ya hiyo Hospitali ya Mkoa, Serikali ina mpango gani sasa wa kutujengea wodi ya watoto katika Hospitali ya Frelimo na wodi ile ya Internal Medicine kwa ajili ya wagonjwa wa kawaida katika Hospitali ya Frelimo pamoja na kututengenezea zile rooms za reproductive health pharmacy na CT katika Hospitali ya Frelimo ili kupunguza changamoto ya Hospitali ya Mkoa wa Iringa?
Mheshimiwa Spika, pia ule mgao tulioomba kwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa; je, tumepata Madaktari? Maana tulikuwa tuna upungufu wa watumishi karibu 200; ahsante sana.
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwenye suala lake la kwanza la ujenzi wa wodi ya akina mama na Watoto, kama ambavyo Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu alisema, katika ununuzi wa vifaa na manunuzi yote ambayo yamefanyika kwa ajili ya vitu mbalimbali kwenye fedha ambazo Rais wetu alitupa, shilingi trilioni 1.3, imeokolewa shilingi bilioni 13, kwa maana tumenunua kwa bei rahisi zaidi kuliko ilivyotegemewa.
Mheshimiwa Spika, sisi na Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo tumezoea kukaa pamoja, tunaweza tukakaa tuone kipaumbele tushirikiane na Waziri wa TAMISEMI ili anachokisema kiweze kufanyika.
Mheshimiwa Spika, suala lako la pili linazungumzia masuala ya Hospitali yake ya Mkoa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, wakati tunakuja na ile timu, mimi naye tutakuwa pamoja na nina uhakika kwamba anachokifikiria kitakwenda kutekelezwa, ahsante.
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza:- Je, ni lini ombi la kubadilishana Hospitali ya Mkoa na ya Wilaya litafanyiwa kazi kuruhusu upanuzi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Kwa kuwa Serikali ilikubali ombi la kupandisha hadhi Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe ya Nansio kuwa na hadhi ya Rufaa ya Mkoa, na tayari imetoa fedha fedha Shilingi bilioni tatu na ujenzi umeanza, lakini kuna sintofahamu kubwa inayosababisha wananchi wa Ukerewe kuwa na hofu kama matarajio yao yatafikiwa na thamani ya fedha ile kweli itafikiwa: Nataka kupata kauli ya Serikali, mnasemaje juu ya hili kuhakikisha kwamba matarajio ya wananchi wa Ukerewe na thamani ya fedha ile kweli inapatikana? Nashukuru sana. (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo Mbunge anakumbuka yeye mwenyewe alifika Wizarani, tukakaa mimi na yeye na Mheshimiwa Waziri wa Afya. Mheshimiwa Waziri wa Afya ameshaunda timu imekwenda Ukerewe kwa ajili ya kuangalia kitaalam ni nini hasa kinaleta sintofahamu hasa kwenye mahesabu. Pia ameshanielekeza, mimi na yeye tutakwenda, nitamchukua yeye twende pamoja baada ya kuchukua ile ripoti ya kitaalam tujadili na Baraza la Madiwani na wataalam ili tufikie muafaka ambao utafanya shughuli zilizoko pale ziweze kuendelea.
Mheshimiwa Spika, vilevile tayari wameongezewa zaidi ya Shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kujenga yale maghorofa ambayo walitamani yajengwe eneo lile.
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza:- Je, ni lini ombi la kubadilishana Hospitali ya Mkoa na ya Wilaya litafanyiwa kazi kuruhusu upanuzi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa?
Supplementary Question 3
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa Kata ya Masama Kati tayari tulishatenga eneo kwa maana ya Kituo cha Afya chenye hadhi ya Kituo cha Afya na wewe mwenyewe umeshafika pale, na tayari tumeshatenga fedha ya kujenga OPD: Je, ni lini Serikali itatuletea fedha ya kumalizia majengo hayo yaliyobaki ambayo pia ni ahadi yako kama sehemu ya Serikali?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, nipokee ombi la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe. Nafahamu tulishafanya ziara kule pia, tukaenda kwa Nsila, tumeanza ujenzi wa Kituo cha Afya kwa Shilingi milioni 250, nafikiri zinaongezeka nyingine. Hicho tutaenda kukifanyia tathmini kuona kama kinakidhi vigezo vya kujenga Kituo cha Afya tuweze kupeleka fedha kwa awamu, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved