Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Je, lini mradi wa maji wa vijiji 57 ambao utaanzia Kyerwa, Nyakatuntu mpaka Kimuli Wilayani Kyerwa utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuulizwa maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais alitoa magari ya kuchimba visima kwenye kila mkoa, lakini magari haya yamekuwa yakienda kila wilaya yanachimba aidha visima viwili, vitatu na kuondoka. Kwa mfano kama Kyerwa tulipewa visima 16 lakini gari lilipokuja lilichimba visima vine;

Je, ni kwa nini magari haya yanapoenda kwenye wilaya yasikamilishe kazi ya kuchimba visima vyote ambavyo vimeainishwa ili kuondoa adha ya usumbufu unaojitokeza?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mradi wa Lutunguru, Kaisho mpaka Isingiro unajengwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza mkandarasi anajenga lakini mpaka sasa hivi anadai zaidi ya milioni 600 ili kukamilisha mradi huu;

Je, ni lini mkandarasi huyu atalipwa ili awamu ya pili iweze kuanza na kuondoa adha inayojitokeza kwa wananchi wangu?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante; naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, gari likifika eneo la tukio likamilishe kazi. Katika kikao cha wiki iliyopita Mheshimiwa Waziri Aweso tayari ameshawaagiza watendaji wote mikoani kulitekeleza hili; na hii ni baada ya Mheshimiwa Waziri Mkuu pia kujionea hali iliyokuwepo pale Lindi. Kwa hiyo tayari kama Wizara tumeendelea kujipanga kuhakikisha kwamba ikifika wakati basi hata tuweze kufanya kazi kikanda. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge Bilakwate nikupongeze kwa maono yako haya ambayo tayari Wizara inafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, awamu ya kwanza ya mradi ipo asilimia 80 na tunaelekea kukamilisha. Madai ya wakandarasi pamoja na mkandarasi huyu anayefanya kazi mradi huu tumeanza kupata fedha na tunaendelea kuanza kulipa kwa mafungu. Kwa hiyo nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge, nikupongeze kwa kufuatilia na madai haya tutakwenda kulipa ili kazi ziweze kuendelea. (Makofi)

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Je, lini mradi wa maji wa vijiji 57 ambao utaanzia Kyerwa, Nyakatuntu mpaka Kimuli Wilayani Kyerwa utaanza?

Supplementary Question 2

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Kwa kuwa gari la kuchimba visima lililoletwa katika Mkoa wa Lindi halijawahi kufika katika Wilaya ya Kilwa;

Je, ni lini gari hili litaletwa Kilwa ili liweze kuchimba visima?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Francis kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu gari kufika Kilwa Mheshimiwa Waziri ameshaagiza lile gari likafanye kazi. Tutaendelea kumuelekeza RM Lindi ili Kilwa nanyi muweze kunufaika na gari lile.