Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bupe Nelson Mwakang'ata
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mgogoro wa Shamba la Gereza la Mollo – Rukwa?
Supplementary Question 1
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nishukuru kwa majibu ya Serikali lakini kimsingi mgogoro huu bado haujaisha na juzi Mwenezi wa Taifa Comrade Makonda, alikuja katika Mkoa wa Rukwa, wananchi wale waliandamana wakishika mabango kwamba wanaomba awaunganishe na Mheshimiwa Rais ili awasaidie kutatua mgogoro huu. Kwa hiyo mgogoro huu bado kabisa ni mbichi wananchi wamelima mashamba na wanakatazwa kwenda kupalilia mahindi yao. (Makofi)
Je, ni lini sasa Serikali itamaliza mgogoro huu?
Swali la pili, Mheshimiwa Waziri upo tayari kuongozana na mimi Bunge hili likiisha ili uweze kwenda kujionea hali halisi ilivyo? Ahsante. (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nipokee malalamiko ya Mheshimiwa Mbunge, kama wapo wananchi ambao wameendelea kulalamika kwamba kuna tatizo la mpaka tutafuatilia kwa karibu ili kuona hatma yake. Kwa vile ameomba niongozane naye naweka ahadi mbele yako kwamba baada ya Bunge hili tutaongozana pamoja na wataalam wa Jeshi la Magereza ili kwenda kujiridhisha ni kitu gani kipo ili tuweze kuumaliza kabisa. Nashukuru. (Makofi)
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mgogoro wa Shamba la Gereza la Mollo – Rukwa?
Supplementary Question 2
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa Gereza la Keko lipo katikati ya makazi ya watu katika Jimbo la Temeke na linaleta migogoro sana kwa baadhi ya nyumba ambazo zinazunguka gereza hilo.
Je, nini mkakati wa Serikali kulihamisha gereza lile kutoka Keko? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Gereza la Keko kama lilivyo kwa sasa Dar es Salaam limezungukwa sana na wananchi na tunatambua hizo changamoto anazozisema. Kwa wakati huu ambapo bado Wilaya ya Temeke halijapata eneo lingine la kulihamishia gereza hilo na hivyo kuliingiza kwenye mpango wetu wa ujenzi wa gereza jipya. Niwaombe wananchi Jeshi la Magereza ni sehemu ya chombo cha wananchi kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kikatiba hayo ya kuhifadhi wenzetu wanao tuhumiwa na kuhifadhiwa kule kwa makosa mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba waishi nao kwa mahusiano mema kabla hatua ya kulihamisha gereza hilo kuliweka eneo la mbali kabisa na makazi ya wananchi. Nashukuru. (Makofi)
Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mgogoro wa Shamba la Gereza la Mollo – Rukwa?
Supplementary Question 3
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Polisi waliopo Itigi wana mgogoro na Shirika la Reli ambalo linajiimarisha sasa na Wizara yake imekuwa na ahadi nyingi kujenga Kituo cha Polisi Itigi, Mheshimiwa Naibu Waziri, mara nyingi tumeongea kuhusu hili. Je, ni lini sasa mtaenda kujenga Kituo cha Polisi kwa ajili ya Polisi wazuri ambao wapo katika Halmashauri ya Itigi? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua na nimshukuru kwa kweli Mheshimiwa Mbunge, kwa namna anavyofuatilia umuhimu wa kuwa na Kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya eneo la Itigi. Nimuahidi tu kwamba kwa vile Eneo la Itigi tayari tumeliweka kwenye mipango yetu avumilie pale Wizara ya Fedha itakapokuwa imetupatia fedha kwa ajili ya kujenga Kituo hicho cha Polisi tutakuwa tumemaliza kabisa mgogoro huo. Nashukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved