Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:- Je, ni hatua gani zimechukuliwa kwa Halmashauri zisizonunua mafuta ya watu wenye Ualbino?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na ninaipongeza kwa hatua ambazo zimeendelea kuchukuliwa. Kwa mujibu wa jibu la msingi inaonesha kwamba katika vipindi viwili vya mwaka (2021/2022) na (2022/2023) imetengwa jumla ya milioni 47 kwa Halmashauri 41.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hesabu ya haraka haraka kwa bei ya 15,000 ya mafuta unapata kwamba ni mafuta 76. Sasa Serikali imesema kwamba ilishatoa maelekezo mwaka 2021. Itakumbukwa kwamba Bunge la Bajeti mwaka 2022, Serikali ilitoa maelekezo na ikasema kwamba itatilia mkazo upatikanaji wa mafuta haya.

Je, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba mafuta haya yanapatikana kwa utoshelevu uliopo ama kwa mujibu wa idadi ya watu wenye ualbino nchini?

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali ilitoa maelekezo kuhakikisha kwamba Halmashauri zote kwanza, zinaainisha na kuwatambua watu wenye ualbino katika maeneo yao; na pili kutenga fedha kwa ajili ya kununua mafuta hayo na kuyagawa kupitia vituo lakini pia katika ofisi mbalimbali za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ambayo tulipata ni kwamba baadhi ya maeneo walikuwa hawajakamilisha tathmini na utambuzi wa watu wenye ualbino ili waweze kujua mahitaji ya fedha zinazotakiwa kutengwa kwa ajili ya mafuta yao. Kwa hiyo tuliwapa maelekezo hayo na tayari halmashauri 41 zilitenga. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mwaka ujao wa fedha tutaweka kipaumbele na msisitizo mkubwa zaidi kuhakikisha kwamba Halmashauri hizi zinatenga fedha kwa ajili ya mafuta ya watu wenye ualbino.

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:- Je, ni hatua gani zimechukuliwa kwa Halmashauri zisizonunua mafuta ya watu wenye Ualbino?

Supplementary Question 2

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni upi mkakati wa Serikali katika kuhamasisha uwekezaji katika viwanda wa kuzalisha mafuta ya ualbino ili kuleta unafuu wa bei?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Toufiq, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya vipaumbele vya Serikali ni kuhakikisha kwamba inaendelea kuhamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje katika uwekezaji wa maeneo mbalimbali na tuna mazao ya aina mbalimbali, tuna mazao ya parachichi na mengine ambayo yanaweza yakazalisha mafuta. Kwa hiyo, kwanza tutumie fursa hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeshaendelea kuboresha mazingira ya wawekezaji; hivyo tunatoa wito kwa wawekezaji ambao wana uwezo wa kutengeneza mafuta hayo ya kusaidia wenzetu wenye ualbino basi watumie fursa ambazo zipo katika maeneo yetu mbalimbali waweze kuzalisha ili tuwe na uwezo wa kuwa na mafuta hayo kwa wingi ndani ya nchi yetu; na Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili yao. (Makofi)