Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Walimu wa kutosha katika Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Kagera?

Supplementary Question 1

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali imefanya kazi nzuri sana ya kupanua elimu msingi na hivyo wanafunzi wameongezeka kwa wingi lakini ongezeko hili halikwenda sambamba na ongezeko la walimu. Kwa sasa Mkoa wa Kagera tuna upungufu wa walimu wa sekondari asilimia 31 na wa sekondari tuna upungufu wa walimu 7,607.

Je, ni lini Serikali itaajiri walimu wengi kwa pamoja ili kuondoa tatizo hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ili tufikie uchumi unaoendeshwa kwa sayansi na teknolojia tunahitaji tuwe na walimu wa kutosha wa sayansi na hisabati.

Je, ni lini Serikali itaajiri walimu wa kutosha kwenye shule zetu hasa za sekondari, walimu wa sayansi na hisabati?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, jambo moja nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, ni kwamba Serikali chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua changamoto ya walimu nchini na ndiyo maana kila mwaka Serikali imekuwa ikijitahidi kuajiri. Ndiyo maana hata mwaka wa fedha unaokuja Serikali itaendelea kuajiri, ambacho tunasubiria ni kibali cha utumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo lini tutaajiri kwa pamoja na kwamba, Serikali itaendelea kuajiri kwa awamu kulingana na bajeti na upatikanaji wa fedha hilo ndio jibu la ukweli kabisa ambalo halina changamoto yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali la pili, kuhusu walimu wa sayansi na wenyewe tutaendelea kuajiri katika kila mwaka tutakuwa tunatenga walimu wa sayansi pamoja na walimu wa masomo ya arts, ahsante sana.

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Walimu wa kutosha katika Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Kagera?

Supplementary Question 2

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa wenye sifa ya kuajiriwa wapo, changamoto ni kuajiri. Wilaya ya Nkasi peke yake tuna changamoto, upungufu wa walimu 855. Ni lini sasa mtawaajiri kwa kuwa wenye sifa wapo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kama nilivyojibu katika swali la awali la msingi pamoja na la nyongeza; ni kwamba tunatambua kwamba wapo walimu ambao wana sifa na bado hawajaajiriwa na Serikali inaendelea kuajiri kulingana na kibali tunachokipata utumishi na bajeti. Kwa hiyo hivi vitu vyote vinakwenda sambamba, hatuajiri tu kwa sababu idadi ya walimu wako mtaani. Tunachozingatia ni mahitaji ya msingi na sisi hilo tunaliona. Kwa hiyo, kadiri uchumi utakavyoendelea kuimarika tunaweza tukaajiri wote kwa wakati mmoja, hilo ndio naweza kulijibu.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Walimu wa kutosha katika Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Kagera?

Supplementary Question 3

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa mikoa ya pembezoni ina tatizo kubwa sana la kupata watumishi wanaoajiriwa na Serikali; Wilaya ya Tanganyika ina tatizo la upungufu wa walimu shule za msingi 1000 na shule za sekondari una upungufu wa walimu zaidi ya 200.
Je, ni lini Serikali sasa itaweka kipaumbele kupeleka mikoa yote ya pembezoni ambayo haipati walimu wa kutosha?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana nimweleze tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, Ofisi ya Rais TAMISEMI ilishatoa majibu. Moja, huwa tunazingatia maeneo yenye uhitaji mkubwa ambao tukiona maeneo hakuna walimu wa kutosha ndipo ambako wanapelekwa lakini mikoa ya pembezoni ni sehemu ambayo inapewa kipaumbele kila ajira mpya zinapokuwa zinajitokeza. Pili, Ofisi ya Rais, TAMISEMI ilishatangaza hadharani kufanyika msawazisho katika maeneo ambayo kuna walimu wengi kupeleka katika maeneo ambayo walimu hawapo wa kutosha, ahsante sana.

Name

Agnes Mathew Marwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Walimu wa kutosha katika Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Kagera?

Supplementary Question 4

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mkoa wa Mara ni mkoa unaotakiwa uwekwe kimkakati na haswa ukizingatia koo zetu kipindi cha nyuma watoto wa kike walikuwa hawasomeshwi na sasa wameamka wameamua kuwasomesha watoto wa kike.

Je, ni lini Serikali itaangalia kupeleka walimu wengi katika shule za sekondari na msingi katika Mkoa mzima wa Mara?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kama nilivyojibu awali ni kwamba, Serikali inazingatia mahitaji katika maeneo yote nchini ambayo kuna uhaba mkubwa, ikiwemo Mkoa wa Mara ambako Mheshimiwa Mbunge ameeleza. Katika kuona ule mwamko wa watoto wa kike Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliamua kujenga shule za kimkakati kila mkoa kwa ajili ya watoto wa kike tu peke yake; yote ni kutaka kuwainua wasichana nchini ili waweze kujikita katika masomo ya sayansi. Kwa hiyo nimhakikishie tutaendelea kuajiri na kupeleka katika mikoa yote ikiwemo Mkoa wa Mara.