Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mussa Ramadhani Sima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mjini

Primary Question

MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa ajira za kutosha kwa Walimu ili kuondoa upungufu uliopo?

Supplementary Question 1

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu hayo ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kwa wako walimu wengi wanaojitolea kwenye shule zetu hizi na hawapati ujira wowote ambao ungewasaidia kujikimu.

Je, Serikali haioni haja sasa kutoa mwongozo kwa wakurugenzi ili watoe ajira za muda mfupi kuwawezesha walimu hao kuweza kujikimu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kwa kuwa upo upungufu mkubwa sana wa walimu wa masomo ya sayansi hasa physics na huko nyuma tunafahamu kwamba Serikali ilikuwa ikitoa crash program mafunzo kwa muda mfupi.

Je, haioni umefika wakati wa kuweka mkakati wa kutoa mafunzo kwa muda mfupi kwa vijana waliomaliza kidato cha sita?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli kwamba Serikali inatambua kwamba kuna walimu wengi wanajitolea katika halmashauri na bado hawapati zile stahili ambazo wanastahili. Kikubwa ambacho nimhakikishie tu kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI ilishatoa mwongozo katika halmashauri zote nchini, kwamba kulingana na mahitaji na makusanyo ya mapato yao ya ndani wanaruhusiwa kutoa ajira za muda. Kwa hiyo niwakumbushe tu Wakurugenzi, kulingana na mahitaji katika maeneo yao waendelee kuzingatia ule mwongozo ambao Ofisi ya Rais, TAMISEMI ulishalitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu walimu wa sayansi ambao wanatakiwa waajiriwe na kwamba tutumie kwamba crash program kwa maana ya mafunzo ya muda mfupi kwa walimu wa form six; kwa sasa hivi bado tuna walimu wengi ambao wanamaliza katika ngazi za elimu mbalimbali wa sayansi na wapo wa kutosha. Kikubwa ambacho sasa hivi Serikali inatafuta ni fedha na kibali ili tuweze kuajiri wote. Naamini hawa tu walioko mtaani tukiwaajiri wote inatosha kabisa kumaliza hii changamoto ya walimu wa sayansi katika shule zetu.

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa ajira za kutosha kwa Walimu ili kuondoa upungufu uliopo?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa Serikali inatambua kuna uhaba wa walimu wa sayansi kwenye halmashauri zetu ikiwepo kwenye Halmashauri za Mkoa wa Morogoro na hapo hapo kuna walimu wengi wa sayansi ambao wako mitaani na wameshaomba ajira lakini hawaajiriwi na huku wana sifa.

Je, Serikali inachukua hatua gani ili kuwaajiri hawa walimu ambao wameshaomba mara nyingi lakini hawaajiriwi na huku wana sifa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, hatua ambayo Serikali tumechukua ni kwamba Ofisi ya Rais TAMISEMI imeomba kibali Ofisi ya Rais, Utumishi; na tukishapata hicho kibali maana yake walimu hao wataajiriwa na tutakuwa tumeajiri kulingana na mwaka wa fedha na bajeti ambayo itakuwa imepatikana, ahsante.

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa ajira za kutosha kwa Walimu ili kuondoa upungufu uliopo?

Supplementary Question 3

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa ajira wakati huu watu wengi wanahitaji na kumekuwa na tabia sasa ya wanafunzi waliomaliza 2015, 2016 kutoajiriwa na wanaajiriwa wa 2021.

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba wale wa miaka ya zamani wanaajiriwa kwa sababu muda wa umri wao unakwenda?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, jambo moja ambalo Mheshimiwa Mbunge ajue kwamba moja ya vigezo ambavyo Ofisi ya Rais TAMISEMI inatumia katika kuajiri walio mtaani ni pamoja na wale wa miaka ya nyuma. Kwa hiyo hilo limekua likitekelezeka na bahati nzuri hata mimi nilikuwa huko kwa hiyo nalifahamu. Tumejitahidi kuajiri walimu kuanzia 2010 mpaka 2016 na baadhi ya miaka hii ya mbele especially walimu wa sayansi, kwa hiyo hilo linazingatiwa katika ajira, ahsante.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa ajira za kutosha kwa Walimu ili kuondoa upungufu uliopo?

Supplementary Question 4

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kuna shule mpya imejengwa kwenye jimbo langu Shule Nsanzate, Shule ya Tingirima na Shule ya Mariwanda zina walimu watatu na shule mpya. Serikali ina mpango gani sasa wa kupeleka walimu pale ilii kuzi-boost hizi shule mpya?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kulingana na maelezo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyatoa hapa tumwagize tu Afisa Elimu Mkoa wa Mara afanye msawazo kuhakikisha kwamba wanaongeza idadi katika shule ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja ikiwemo Nsanzati, Tingirima ili sasa waweze kuwa katika ile ikama inayohitajika, ahsante. (Makofi)