Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tecla Mohamedi Ungele

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TECLA M. UNGELE K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, kwa nini baadhi ya miradi inayoibuliwa na jamii kupitia TASAF hukataliwa na kutekelezwa miradi ambayo haikuibuliwa na jamii?

Supplementary Question 1

MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu ya Serikali nina swali la nyongeza.

Kwa kuwa jamii yetu bado elimu hii ya uibuaji miradi yenye tija haijaeleweka vizuri. Je, Serikali ina mkakati gani wa kupeleka elimu hii kwa jamii na elimu hiyo iwe endelevu? Ahsante. (Makofi)

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na jambo la elimu kwamba haijaenea vizuri kwa wananchi, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako kwamba, katika utaratibu wa mikutano ile mikuu ya Vijiji, Kata au Shehia ambayo inakwenda kuibua miradi, hatua ya kwanza wanayofanya wataalam wetu ni kuendelea kuelimisha kwanza wananchi kabla hawajaibua miradi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shida kubwa ambayo inatokea ni kwamba wananchi wanakuwa na vipaumbele vyao dhidi ya ile mipango ambayo Serikali inaileta, kwa hiyo, hapo ndipo pamekuwa na tatizo na mgongano wa mara kwa mara. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi wetu ili kuhakikisha kwamba wanafika sehemu wanaibua miradi ambayo inaendana moja kwa moja na changamoto zilizopo katika maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji.