Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na kuimarisha soko la bidhaa?
Supplementary Question 1
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kushukuru sana Serikali na majibu ya Waziri, kwa kweli yanaleta matumaini kwa wakulima hasa kutokana na kuongeza tija lakini pia kwa kuwaunganisha wakulima moja kwa moja kwa wanunuzi wa nje na wa ndani.
Swali langu la kwanza, kwa sababu kuna hizi fursa, je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha kuwa inaongeza mazao hasa yale mazao ambayo ni adimu duniani kama pareto au madini ambayo yanapatikana Tanzania tu? Ina mkakati gani wa kuongeza hayo mazao na hayo madini kwenye hili soko ili Watanzania waweze kunufaika?
Swali la pili, kwa vile kuna hizo fursa ambazo wanunuzi wengi kwa sasa hivi ni madalali na inawezekana siyo Watanzaia, wanaingia mikataba na Watanzania kwa pesa za Tanzania na wao wanafaidika kwa pesa za kigeni. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwalinda hawa wakulima ambao wamekuwa wakinyonywa kwa muda mrefu kutokana na mabadiliko, hasa ya kupungua kwa thamani ya shilingi? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Katika swali lake la kwanza la nyongeza kwamba, je, Serikali tumejipangaje kuongeza idadi ya mazao, kwa mfano ametolea pareto na baadhi ya madini. Nimhakikishie tu kwamba, huo ndiyo mpango wa Serikali na tunafanyia kazi. Katika mwaka wa fedha wa bajeti unaokuja tutatangaza mazao gani yataingia katika soko la bidhaa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu ni namna gani tunaweza kuwasaidia wakulima kutokana na mabadiliko ya thamani ya shilingi. Niseme tu jambo hili ni suala la Sera ya Fedha (Monetary Policy) na linasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, sisi kama Wizara ya Kilimo tutashirikiana na Wizara ya Fedha, tutakaa pamoja na kuona namna bora ya kuwasaidia wakulima wetu nchini. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved