Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanzisha Kituo cha Madume Bora ya Ng’ombe Wilayani Bahi?

Supplementary Question 1

MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naishukuru sana Serikali kwa ahadi ya kunipatia madume 20 ya ng’ombe katika mwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza. Kiasi hiki cha madume 200 ambayo Serikali inanunua ukilinganisha na idadi ya ng’ombe tuliyonayo ni hatua kidogo sana. Kwanza, hata hayo madume yenyewe tunayachosha kwa maana ya wingi wa majike yaliyopo. Je, Serikali haioni kwamba badala ya kununua madume 200 tuongeze tufike angalau hata 1,000 ili nchi nzima katika maeneo ya wafugaji tuweze kupata madume mengi na kwa uhakika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Dodoma tuna Kituo cha Utafiti wa Malisho pale Mpwapwa na hapa Kongwa, lakini ukija katika Wilaya yangu ya Bahi kwenye kata za wafugaji ukianzia pale Chifutuka, Chipanga na Chikora, hakuna hata nyasi moja ya utafiti ambayo imeletwa katika wilaya yetu. Je, Serikali ina mpango gani wa vituo hivi ambavyo vina miaka mingi, lakini taarifa zake na matunda yake hayafiki katika wilaya zinazovizunguka? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hili la madume 200. Ni kweli madume 200 ni wachache na mpango wa Serikali ni kuongeza kadri ya upatikanaji wa bajeti. Tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tuko tayari kuongeza madume hao kadri ambavyo bajeti inapatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu hili la nyasi, tayari wataalam wetu wanaendelea na utafiti katika maeneo mbalimbali ya nchi, ukiwemo Mkoa wa Dodoma. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mara tu utafiti utakapokamilika, basi mbegu za nyasi bora zitakwenda katika Jimbo lake la Bahi. Kwa sasa watafiti wetu wanafanya utafiti katika maeneo mbalimbali ikiwa ni Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Dodoma na maeneo mengine, na Bahi pia watafika kwa ajili ya kukamilisha utafiti huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutakuja Bahi kwa ajili ya kukamilisha utafiti huo na majibu yatakapopatikana, wataalam wetu wako tayari kutoa elimu kwa wafugaji wetu ili waweze kutumia nyasi hizo zinazotakiwa. Ahsante.

Name

Catherine Valentine Magige

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanzisha Kituo cha Madume Bora ya Ng’ombe Wilayani Bahi?

Supplementary Question 2

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itajenga Kiwanda cha Nyama na Malighafi za Mifugo Wilayani Ngorongoro kwa kuwa 80% ya wananchi katika wilaya hii ni wafugaji? (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ujenzi wa Kiwanda cha Nyama, Serikali inaendelea kuhamasisha wawekezaji mbalimbali katika maeneo mbalimbali ili kuwekeza katika sekta hii kwa sababu imeonekana viwanda hivi vina tija katika mazingira hayo. Kwa hiyo, tunamwomba Mheshimiwa Mbunge pia kama ana mawasiliano na wadau mbalimbali katika maeneo mbalimbali wanaoweza kuwekeza katika sekta hii, pia tuko tayari kushirikiana nao katika kuhakikisha kwamba viwanda hivi vinapatikana katika Taifa letu. Ahsante.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanzisha Kituo cha Madume Bora ya Ng’ombe Wilayani Bahi?

Supplementary Question 3

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, nini mpango wa Serikali kwa vikundi vya wafugaji wa Simanjiro, Kiteto na Hanang kuleta mbegu ya madume bora?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi, ni kwamba madume bora yapo na katika bajeti ya mwaka huu pia tutaongeza idadi ya madume bora, na Wilaya ya Hanang, Kiteto, Simanjiro na maeneo mengine kote ambako wanahitaji madume bora, tuko tayari kuwapelekea. Ahsante.

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanzisha Kituo cha Madume Bora ya Ng’ombe Wilayani Bahi?

Supplementary Question 4

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa bei ya madume bora wamekuwa ni ghali sana hasa kwa hawa wa Serikali, kwa nini Serikali isipunguze bei sana ili wafugaji waweze kununua?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli madume hawa bei yake ilikuwa iko juu. Ilikuwa ni shilingi 4,000,000/= mpaka shilingi 6,000,000/=, lakini kwa concern hiyo ya Mheshimiwa Mbunge, pia madume hao wameshashuka bei. Sasa madume hao wanapatikana kwa shilingi 1,000,000/= mpaka shilingi 1,500,000/=. Kwa hiyo, Serikali inaendelea kupokea ushauri kama bei hiyo pia itakuwa bado inawatatiza wafugaji wetu, tuko tayari kuishusha na kuona namna ambavyo tutawasaidia wafugaji wetu katika maeneo mbalimbali. Ahsante. (Makofi)

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanzisha Kituo cha Madume Bora ya Ng’ombe Wilayani Bahi?

Supplementary Question 5

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mpango mzuri wa Serikali wa kuhakikisha kwamba, madume bora wanapatikana, lakini ni ukweli usiopingika kwamba wapo ng’ombe wa asili, kwa mfano wenye asili ya Wafipa ambao wanapatikana ndani ya Mkoa wa Rukwa ambao size yake ni kubwa na wanafanya vizuri kama wanyamakazi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba hatupotezi specie hii ambayo ni nzuri?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendelea kuhamasisha ufugaji wa kisasa, na hawa ng’ombe wa asili anaowasema Mheshimiwa Mbunge kama wataonesha kuwa na tija, tuko tayari kuwalinda, lakini kusema kweli kwa sasa Wizara inajikita zaidi kwenye kuhamasisha ufugaji wa kisasa, wenye tija, wenye kutumia eneo dogo na kwa faida kwa ajili ya wafugaji wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wataalam wanaendelea kufanya uchunguzi wa jambo hili na ikionekana mbegu hizi za Wafipa zina faida kwa wafugaji wetu, tuko tayari kuzilinda na kama zinaonekana hazina faida, ni vizuri wafugaji wetu wakajifunza kufuga kisasa kwa ajili ya faida yao ya baadaye. Ahsante. (Makofi)