Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza:- Je, kuna fursa na changamoto gani kwa Tanzania kushiriki kwenye biashara ya carbon.

Supplementary Question 1

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali.

Swali la kwanza; sasa kutokana na hizo changamoto alizozisema Mheshimiwa Waziri kuna makubaliano ya Paris na Article 6, imewezesha nchi kwa nchi kufanya biashara na nchi nyingi zikiwemo Nchi za Afrika Mashariki zimefaidika kupitia hilo. Wenzetu majirani wameweza kuwekeza kwenye hekta 100 na wamezalisha ajira takriban 200,000. Je, Serikali ina mpango gani wa kutumia Soko la Mitaji (Capital Market Authority) ili iweze kuweka regulation na kuweza kuleta wawekezaji kutoka nje ambao wako tayari kuja kuwekeza hapa kwetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa sababu imeonesha kuwa uwekezaji katika biashara ya kaboni umesaidia sana kwenye kilimo kupunguza mbolea. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa maeneo kama ya Nyanda za Juu Kusini inawekezwa biashara ya kaboni ili tupunguze matumizi ya mbolea na tuongeze uzalishaji wa mazao? Nashukuru sana.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oran, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nataka nimpongeze sana Mheshimiwa Oran kwa maono yake mazuri na hasa katika eneo hili jipya la biashara ya kaboni.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2022 tulitengeneza kanuni za kwanza, tulikuwa watu wa kwanza katika East Africa kuwa na kanuni, lakini kutokana na utekelezaji wa Article 6 ya Paris Agreement mwaka 2023 tulifanya rejea katika eneo hilo. Hivi sasa, kama nilivyosema juzi hapa kwamba zaidi ya miradi 42 imeshasajiliwa. Sasa hivi tuko katika mchakato na baadhi ya maeneo kampuni nyingine sasa zimeonesha hali ya kutaka kwenda katika eneo hilo. Kwa hiyo naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumejipanga vizuri kwa upande wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la uwekezaji katika Nyanda za Juu Kusini, naomba niwahakikishie, miongoni mwa kampuni hizi 42 nyingine zime-identify miradi katika eneo hilo. Kwa hiyo imani yetu kubwa ni kwamba miradi hii sasa itakayotekelezwa katika maeneo mbalimbali italeta manufaa makubwa sana, hususan katika nyanda za juu kusini. Ahsante sana.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza:- Je, kuna fursa na changamoto gani kwa Tanzania kushiriki kwenye biashara ya carbon.

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa wanunuzi wa carbon kwa Tanzania asilimia kubwa ni middleman, ambao wanatulipa fedha kiduchu kuliko zile ambazo ni stahiki. Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuwapata wanunuzi wa moja kwa moja kuliko walivyo sasa hivi tunaopata hawa ambao ni middleman? Tunaomba kufahamu. (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, Mbunge wa Tanganyika, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Kakoso, katika watu ambao wamekuwa aggressive katika maeneo yao katika biashara ya carbon ni Mheshimiwa Kakoso. Tunakumbuka kwamba hivi karibuni Halmashauri ya Tanganyika ilikuwa ikipata fedha kadhaa na gawio la mwisho ilikuwa imepata karibuni three point something billions, lakini kutokana na huo uhitaji na nguvu kubwa mwaka huu expectation wataweza kupata kati ya shilingi bilioni 10 mpaka shilingi bilioni 14.7, kwa hiyo, Mheshimiwa Kakoso hongera sana katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kufanya hilo sasa Serikali ndiyo maana imetengeneza kanuni, katika kanuni ya 4(2) inazungumzia issue ya transparency. Lengo letu ni nini, katika eneo hili watu wanaotoa credit zao hapa nchini watakapokwenda katika stock exchange lazima ku-declare kwamba wametoa ngapi na wameuza ngapi, kwa lengo la kuhakikisha mahitaji halisi hasa ya kifedha yanawafikia watu ambao wanatunza rasilimali za misitu katika nchi yetu, ahsante sana. (Makofi)

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza:- Je, kuna fursa na changamoto gani kwa Tanzania kushiriki kwenye biashara ya carbon.

Supplementary Question 3

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Halmashauri ya Masasi imekuwa na elimu ndogo kuhusiana na jambo hili. Je, Serikali ina-commitment gani kuhakikisha inatupa elimu hii, hususani katika Jimbo langu la Lulindi? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mchungahela, Mbunge wa Lulindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli nimesema kuna gap kidogo, suala la uelewa na ndiyo maana Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, iliamua kutafuta fursa ya kutoka kwa wadau kwa ajili ya kufanya capacity building kwa wataalamu wetu. Ndiyo maana sasa hivi Serikali kupitia Shirika la UNEP tutaenda kufanya awareness na capacity building kwa wataalamu wetu wa mazingira katika halmashauri zetu, Lengo kubwa tuwe na uelewa mzuri katika suala zima la uwekezaji katika biashara ya carbon. Kwa hiyo, kwenye hilo ni kwamba hata wataalamu wa Lulindi watapata fursa hiyo kupitia uhusiano huu tuliokuwa nao na UNEP. Ahsante sana. (Makofi)