Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MH. ALLY J. MAKOA aliuliza:- Je, lini umeme wa REA utapelekwa Mitaa ya Chemchem, Tampori, Kwamtwara, Guluma, Mongoroma, Chandimo, Chang’ombe na Tura?

Supplementary Question 1

MH. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali yenye kutupa matumaini naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; baada ya Serikali kutupatia katika kipindi hiki hiyo mitaa 15, vipi sasa kuhusiana na ile mitaa ambayo haikutajwa hapo ambayo imebaki mfano Chora, Damai, Ngereli pamoja na Hurumbi na yenyewe mpango wao ukoje?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, ni lini Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kufuatana na mimi twende Kondoa kwa ajili ya kuona yale mazingira na namna watu wanavyohitaji huo umeme. Nashukuru. (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye jimbo lake. Katika mitaa ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge tutazingatia katika bajeti inayofuata kuona kama mitaa mingine imebakia tunaweza kuiingiza baadhi ili kuweza kuwafikishia wananchi huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na kuambatana na yeye jimboni, tutapanga na Mheshimiwa Mbunge siku za hivi karibuni ili tuweze kwenda kuona utekelezaji wa miradi katika jimbo lake, ahsante. (Makofi)