Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Godwin Emmanuel Kunambi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la Mto Kilombero?

Supplementary Question 1

MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

(a) Mheshimiwa Spika, Skimu ya Umwagiliaji ya Njagi ni skimu ambayo haijakamilika na wananchi wameanza kunufaika nayo. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kuhifadhia maji?

(b) Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Mlimba tumelazimika kuishi kwa matumaini, je, sisi wananchi wa Kata ya Utengule, Chisano, Ching’anda, Mgeta, Mchombe na Idete, tungependa kujua ni lini mradi huu utaanza? Ahsante.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mradi wa Skimu ya Njagi umeshaanza na kinachosubiriwa ni bwawa na liko katika awamu inayofuatia, kwa hiyo, nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge, mradi huo upo katika mpango wa ujenzi wa bwawa katika mwaka wa fedha unaokuja. Kwa hiyo, ninaamini utatekelezeka katika kipindi kinachokuja.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa eneo la Kata za Utengule, Chisano, Ching’anda, Mgeta, Mchombe na Idete na zenyewe kwa sababu Mshauri Elekezi yuko site na tumekubaliana kwamba katika next financial year tunaliingiza katika mpango wa bajeti, maana yake tutaanza utekelezaji katika mwaka wa fedha unaokuja, ahsante.

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la Mto Kilombero?

Supplementary Question 2

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini utakuwa tayari kutembelea Halmashauri ya Mji wa Ifakara kujionea maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nipo tayari muda wowote. Tukiomba ruhusa tu kwa Mheshimiwa Spika, hata weekend tutakwenda.

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la Mto Kilombero?

Supplementary Question 3

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Spika, je, katika utekelezaji wa bajeti mwaka huu wa fedha, ni lini Serikali itaanza mchakato wa miradi ya umwagiliaji katika maeneo yaliyo pembezoni mwa Ziwa Victoria Jimboni Busanda ukizingatia imebaki miezi miwili kwenye hii bajeti? Nashukuru sana,

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Miradi mingi ambayo ipo katika mwaka wa fedha wa bajeti uliopo sasa hivi, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea kuitangaza kila wakati na ninaamini kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha tutakuwa tumeshatangaza na kupata mkandarasi.