Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. TABASAM H. MWAGAO aliuliza:- Je, lini mradi wa ujenzi wa Feri ya MV Buyagu utakamilika ikizingatiwa kuwa mkataba wa ujenzi umekwisha muda wake Aprili, 2024?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina masali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza kwa kuwa ujenzi wa kivuko hiki ulikuwa unaenda sambamba na ujenzi wa gati, Gati la Mbarika na Gati la Buyagu, wananchi wa Wilaya ya Sengerema wanataka kujua ni lini sasa gati hizi zitakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Kivuko cha Kisorya kwenda Ukerewe kimekuwa ni hatari sana kwa maisha ya wananchi wa Ukerewe na kwa kuwa kivuko hicho pamoja na Kivuko cha Bukondo Bwiro, Kivuko cha Kome na hiki Kivuko cha Buyagu vyote vilitakiwa kukamilika pamoja; nini kauli ya Serikali ili tusisubiri yakatokea mambo ya kutisha ndiyo tukakurupuka kwenda kufanya shughuli zinazotakiwa pale? Nashukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Gati za Mbarika na Buyagu ziko kwenye mpango wa kujengwa na tutahakikisha wakati tunakamilisha kivuko na gati hizo ziwe zimekamilika ili kivuko hiki kiweze kufanya kati ya pande hizo mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Kivuko cha Kisorya ambacho kina-operate kati ya Kisorya na Rugenzi ikiwa ni pamoja na vivuko vingine, maana tuna vivuko vipya zaidi ya vitano ambavyo vinajengwa na tuna uhakika kwamba pengine kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu vivuko vyote vitakuwa vimeshakamilika kwa sababu vingi viko zaidi ya 75% vikiwa vinajengwa pale Songoro Marine pale Mwanza, ahsante.