Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: - Je, kuna ukweli kwamba kina cha maji ya Bahari ya Hindi hapa Tanzania kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na nini athari zake?

Supplementary Question 1

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa Serikali imekiri kwamba kuna ongezeko la kina cha maji kule baharini, je, Serikali ina mpango gani wa kuyalinda maeneo haya ili yasije yakazama kwenye maji huko siku za mbeleni? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa hili ni tatizo la kidunia, je, Serikali inashirikianaje na wadau mbalimbali wa kimataifa ili kukabiliana na changamoto hii? (Makofi)

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya mtaalam mbobezi, Mtaalam wa Kilimo na Sayansi ya Udongo – Profesa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika kuona hili ndiyo maana mwaka 2021 tulifanya rejea ya Sera yetu ya Mazingira ya mwaka 1997, lakini mwaka 2022 tulikuja na mpango mkakati wa kuona jinsi gani tunashughulikia masuala mbalimbali ya kimazingira ikiwemo na suala hili la uharibu wa mazingira hasa upande wa fukwe. Kwa hiyo katika hili naomba niwahakikishie Wabunge kwamba tumejipanga vizuri na hivi karibuni tunakuja na Sera nyingine mpya ya Blue Economy ambayo itaangalia corridor zote za bahari na jinsi gani tunaweza kuzilinda. Kwa hiyo, Serikali iko mbioni kuhakikisha kwamba tunafanya mambo hayo kwa uhakika wa hali ya juu.

Mheshimiwa Spika, ushirikiano tunafanya vipi? Kwanza tumshukuru sana Dkt. Samia Suluhu Hassan katika agenda yake ya mazingira, tunakumbuka Mkutano wa COP 26 alipokuwa Glasgow alivyotangaza duniani agenda ya mazingira na kufanya resource mobilization kutafuta wadau mbalimbali katika upande huu. Katika hili naomba niwahakikishie kwamba, Serikali ina mahusiano mazuri sasa hivi na UNEP, FAO na UNDP. Pia sasa hivi tuna mchakato mkubwa wa kujiunga na Shirika kubwa la GGI kule Korea kwa lengo kubwa la kuweza kupata fedha ili kusaidia shughuli za maendeleo katika nchi yetu. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: - Je, kuna ukweli kwamba kina cha maji ya Bahari ya Hindi hapa Tanzania kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na nini athari zake?

Supplementary Question 2

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa Serikali ya Mkoa wa Manyara imeendelea kupambana kuokoa kina cha Ziwa Babati na tumeshaomba fedha zaidi ya miaka mitatu na Mheshimiwa Waziri amekuwa akituahidi mara kwa mara…

SPIKA: Swali.

MHE. ASIA A. HALAMGA: Je, nini kauli ya Serikali sasa juu ya kuliokoa Ziwa Babati? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, Serikali inakuja na mpango katika mwaka huu wa bajeti kwa Ziwa Babati na Ziwa Jipe na maeneo mengine kuhakikisha kwamba tuna-address changamoto ya magugu maji katika maeneo haya. Ahsante. (Makofi)

Name

Khalifa Mohammed Issa

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Mtambwe

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: - Je, kuna ukweli kwamba kina cha maji ya Bahari ya Hindi hapa Tanzania kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na nini athari zake?

Supplementary Question 3

MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Spika, je, kuna mpango gani wa kukinusuru Kisiwa cha Mtambwe Mkuu kilichopo katika Jimbo la Mtambwe kuzama?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kule Pemba eneo hili lina changamoto kubwa na ndiyo maana tulituma wataalam wetu sasa hivi kupitia maeneo mbalimbali. Katika hilo ni kwamba tutaainisha nini kifanyike, lakini kubwa tutashirikiana na wananchi wetu katika maeneo mbalimbali hasa kutoa elimu ya kwanza ya jinsi ya kuyalinda maeneo hayo hasa kupanda miti katika maeneo hayo. Hata hivyo tutaenda kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kuta za bahari katika maeneo kama hayo. Ahsante sana.

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: - Je, kuna ukweli kwamba kina cha maji ya Bahari ya Hindi hapa Tanzania kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na nini athari zake?

Supplementary Question 4

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa athari hizi pia zinasababisha theluji iliyopo kwenye Mlima Kilimanjaro kuyeyuka. Je, Serikali ina mpango gani kugawa miche kila siku iitwayo siku kwa wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro ili waendelee kuotesha mgombani?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mama yangu Shally Raymond, Mbunge machachari kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mkoa wa Kilimanjaro tuna changamoto kubwa na hasa kulinda Mlima ule Kilimanjaro na hapa naomba nichukue fursa hii kuwashukuru wenzetu wa TFS wameendelea kufanya kazi hii, naomba nimpongeze Profesa Dos Santos Silayo wa TFS kwa sababu yeye ameamua kuweka nguvu kubwa ya upatikanaji wa miche katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kugawa. Kwa hiyo, nawaomba akinamama wa Mkoa wa Kilimanjaro wawasiliane na TFS kwa maeneo hayo, naamini watapata miti kwa ajili ya kupanda. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Simai Hassan Sadiki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nungwi

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: - Je, kuna ukweli kwamba kina cha maji ya Bahari ya Hindi hapa Tanzania kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na nini athari zake?

Supplementary Question 5

MHE. SIMAI HASSAN SADIKI: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kutambua athari za ongezeko la maji ya bahari zinazoendelea kutokea kule Nungwi?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba kumpongeza Mheshimiwa Simai, kwa sababu mimi na yeye tumefika katika eneo la Jimbo lake pale na kweli kuna changamoto kubwa sana, hata upande wa soko mpaka msikitini pale kuna changamoto kubwa. Sasa hivi Serikali inatafuta fedha mahsusi ili kuhakikisha tunasaidia eneo la Nungwi kwa sababu changamoto yake ni kubwa. Kwa hiyo, Serikali tunaendelea kuhangaikia fedha na wewe nimekuambia kwamba tuna vikao mbalimbali, Mheshimiwa Mbunge nimeongea naye, vikao mbalimbali vya kuangalia namna ya kusaidia specific eneo la Nungwi kutokana na uharibifu unaotokea pale. Ahsante.