Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha uchimbaji wa Mbunyu unatekelezwa katika Kata ya Chiwata - Ndanda? (Makofi)

Supplementary Question 1

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mradi huu ulikusudiwa uanze tangu mwaka 2016 lakini mpaka sasa hivi taratibu zimechelewa kama alivyojibu kwenye majibu ya msingi. Je, ni lini mradi huu utaanza? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, vijiji vinavyonufaika na mradi huo wa Mbunyu, Chiwata na Chidya, vitanufaikaje kutokana na mradi huo utakapoanza? (Makofi)

Name

Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Longido

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la kwanza, naomba nimjulishe Mheshimiwa Mbunge kwamba kama nilivyosema katika majibu ya swali la msingi, sasa hivi off-takers wale wanunuzi wa hiyo graphite ambayo ni kati ya madini mkakati yanayohitajika sasa hivi duniani kwa utengenezaji wa battery na vifaa vya magari yasiyotumia mafuta, yanatumia umeme, ni kwamba wamepatikana wawekezaji hao kutoka Marekani na kutoka Ulaya na wako katika hatua za mwisho ili uzalishaji uendelee.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwa swali lake la pili, faida za mradi huu utakapoanza ni nyingi, kwanza ninawapongeza hawa ndugu zetu wa Volt Graphite kwa sababu hata kabla mradi huu haujaanza, katika upande wa kutoa mchango kwa jamii, wameshachangia fedha katika ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Kijiji cha Nangwale, lakini pia wanachangia posho za walimu wawili wa kujitolea katika shule iliyoko katika kijiji hicho kama sehemu ya kuonesha dhamira yao njema.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia wameanzisha ofisi mbili katika Kijiji hicho cha Nangwale na Chiwata ambazo zinadumisha mahusiano na jamii ile. Ila watakapoanza kanuni zetu zinawataka kupitia kanuni za uwajibikaji na ushiriki wa Watanzania (local content) watoe ajira na wawaruhusu wenyeji na Watanzania kutoa huduma zote muhimu ambazo wanaweza kuzitoa pamoja na CSR sasa ambao wameanza kutoa kabla ya mradi kuanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mradi huu utakuwa na manufaa makubwa na ninawaasa wananchi wa maeneo hayo ya Mradi wa Mbunyu wakae mkao wa kutoa ushirikiano katika kampuni hii ambapo itakapoanza uzalishaji, matunda yake yatasambaa katika jamii husika, ahsante sana. (Makofi)

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha uchimbaji wa Mbunyu unatekelezwa katika Kata ya Chiwata - Ndanda? (Makofi)

Supplementary Question 2

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, wananchi wa Kijiji cha Mpepo kwa muda mrefu hawajaweza kuendelea na shughuli zao kutokana na suala kwamba kuna mwekezaji ilikuwa aendeleze eneo hilo kwa ajili ya uchimbaji na awalipe fidia, lakini imechukua muda mrefu sasa huyu mwekezaji hajaweza kufanya hiyo.

Je, Mheshimiwa Waziri utalichukua hili ili uweze kulifuatilia ili wananchi hawa waweze kuendelea na shughuli zao? (Makofi)

Name

Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Longido

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la wawekezaji kuchelewesha fidia na kusababisha wananchi kutoweza kuendeleza yale maeneo ni suala ambalo linasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini ya mwaka 2016 ambayo inamtaka aliyefanya uthamini ili afidie watu ndani ya miezi sita aanze kuwalipa na asipowalipa alipe fidia kwa kipindi cha miaka miwili na asipolipa uthamini huo unakufa na unaanza upya.

Kwa hiyo, hao wananchi wa Mpepo ambao wamekwamishwa kuendelea na uendelezaji wa maeneo yao kama uthamini umechewa kulipwa na miaka miwili imeshapita, huo uthamini hauna maana tena ina maana utafanywa upya na commitment ya huyu kuendelea na uthamini aweze kuwekeza, sisi kama Wizara tutafuatilia ili tujue kikwazo ni nini na ikibidi sasa aanze uthamini upya ili wananchi wafidiwe ili mradi huo uweze kuendelea.