Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Noah Lemburis Saputi Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kujenga Mahakama Kata ya Bwawani katika Jimbo la Arumeru Magharibi?
Supplementary Question 1
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ambayo yenye mkanganyiko wa kimaeneo, naomba kusema kwamba eneo la Maji ya Chai halipo katika Jimbo la Arumeru Magharibi, lipo katika Jimbo la Arumeru Mashariki. Kwa hiyo, Maji ya Chai siyo Arumeru Magharibi. Jambo lingine, kilometa 15 alizotaja hapa, siyo sahihi. Naomba kwenda kwenye maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa katika maeneo hayo kulikuwepo na changamoto ya kiusalama zaidi na Serikali ikaamua kwa maana ya Jeshi la Polisi kupeleka Kituo cha Polisi katika eneo la Kata ya Bwawani: Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga Mahakama ili kuhakikisha kwamba kuna amani na utulivu katika maeneo hayo na haki ipatikane?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kulikuwepo kuna suala la mradi wa ujenzi wa Mahakama kwa kata ambazo zipo ndani zaidi, na tukaorodhesha ikiwemo Kata hiyo ya Bwawani. Je, mradi huo umekufa au haupo tena?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge, najua tunapozungumzia Majimbo au Halmashauri kwenye upande wa Mahakama huwa tunakwenda kwenye mwelekeo wa kiwilaya ndiyo maana tumeweza kuitaja Wilaya ya Arumeru, lakini nimemwelewa vizuri, tutaweza kuwasiliana na Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kuweka sawa maeneo haya ambayo ameona kama yana mkanganyiko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwepo wa Kituo cha Polisi na hivyo kuhitaji Mahakama. Kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, ni nia ya Serikali kusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi ili waweze kupata haki kwa wakati. Hata hivyo, nia yetu hiyo njema inategemea upatikanaji wa fedha, ndiyo maana Mahakama imekuja na mpango wa ujenzi wa Mahakama katika maeneo mbalimbali. Kadiri fedha zinapopatikana, maeneo hayo yataendelea kufikiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwepo wa kata hizi, ndiyo maana nimemwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba katika bajeti ya mwaka 2026/2027, eneo analolisema tutaweza kulizingatia katika ujenzi wa Mahakama. Nashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved