Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR aliuliza: - Je, lini vyombo vya usafiri vilivyosajiliwa Zanzibar vitatambuliwa Tanzania Bara?

Supplementary Question 1

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mchakato wa mabadiliko ya sheria hii ili kuweza kufanya vyombo vya usafiri kutambulika hapa Tanzania Bara umeonekana umechukua muda mrefu sana, sasa ni kwa nini Serikali haioni haja ya kuweka mwongozo maalumu kipindi hiki wakati tunasubiria mabadiliko ya sheria hiyo?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bakar, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zipo katika mazungumzo, naomba tuwe na subira na utaratibu uliopo kwa sasa uendelee kutumika. Pale mazungumzo yatakapokamilika, basi marekebisho yatafanyika ili kuhakikisha kwamba vyombo vinasajiliwa kwa pamoja.