Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza: - Je, lini Muswada wa Sheria ya Sekta Binafsi ya Ulinzi utaletwa Bungeni kwa kuwa kampuni binafsi za ulinzi zilianzishwa bila sheria wala kanuni?
Supplementary Question 1
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniruhusu niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali na kwamba ninaipongeza sana Serikali kwa kuwa na nia ya kuleta muswada huu hapa Bungeni, nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Jeshi la Polisi limeanzisha Kampuni ya Ulinzi Binafsi, wakati huo huo Jeshi la Polisi ndio wasimamizi wa sekta hii ya ulinzi binafsi, kampuni za ulinzi zinaona kwamba suala la Jeshi la Polisi kuanzisha kampuni ya ulinzi litaleta ushindani mbaya kinyume na matakwa ya Tume ya Ushindani.
Je, Serikali inasema nini kuhusu suala hilo?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Athuman Almas Maige, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kampuni ya ulinzi iliyoanzishwa na aliyosema ya polisi si ya Jeshi la Polisi ni ya Shirika la Uzalishaji la Polisi, ni shirika ambalo linafanya biashara kama shirika lingine. Kwa hiyo, siyo kampuni ya Jeshi la Polisi per-se, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved