Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nancy Hassan Nyalusi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mtaji MSD?
Supplementary Question 1
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; Mheshimiwa Naibu Waziri, hii shilingi bilioni 100 ni mtaji au amelipa deni kwa sababu, kwenye vitabu vya MSD inasomeka kama ni deni?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kumekuwa na changamoto katika usambazaji wa vifaa tiba na dawa. Je, nini kauli ya Serikali? Ahsante.
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, huu ni mtaji na Mheshimiwa Mbunge asisahau kwamba, kila mwezi MSD wanapewa shilingi bilioni 16.7 kwa ajili ya manunuzi ya dawa. Maana yake ni kila mwezi wanapata shilingi bilioni 16.7 na wamepewa hizi shilingi bilioni 100, ambazo wao wameamua kuelekeza kwenye kumalizia ujenzi wa viwanda.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili amezungumzia suala la kwamba, kuna changamoto kwenye usambazaji wa vifaa tiba. Labda hiyo ni habari mpya, lakini hakuna changamoto kwenye usambazaji na ndiyo maana unasikia sasa hivi tumetumia zaida ya shilingi trilioni 6.7 kununua vifaa tiba na umeona vimesambazwa kwenye wilaya mbalimbali na wakati wote dawa zinafika kwenye wilaya mbalimbali. Kama kuna eneo ambalo umeliona lina changamoto, naomba uje kwenye kiti changu tujadili tuone kwa pamoja jinsi ya kulitatua.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved