Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Godwin Emmanuel Kunambi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlimba
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa gati katika Mto Mnyela, kuunganisha Halmashauri ya Mlimba kupitia vijiji vya Ngalimila na Ngombi?
Supplementary Question 1
MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza (a) na (b).
(a) Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hii gati ikikamilika itahitaji pantoni, ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba gati itakapokamilika na pantoni itakuwa pale?
(b) Barabara inayounganisha hiyo gati inayotoka Mpanda kuja hapa Ngalimila, ni barabara ambayo ina mashimo mengi sana, kwa hiyo, haileti mawasiliano pale. Ni nini mpango wa Serikali kuijenga barabara hii ili gati ikikamilika na barabara iwe imekamilika na pantoni iwe pale? Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni kweli kwamba pantoni au kivuko ambacho kitakwenda kwenye eneo hili ni kile kilichokuwa kinafanya kazi pale Kilombero baada ya kujenga daraja. Mkandarasi ambaye amekikarabati hiki kivuko ni Songoro, ambapo baada ya kupata hiyo tenda aliona ni rahisi kwake kufanyia katika karakana yake. Kwa hiyo, alikifungua, na tunavyoongea sasa hivi kipo 95% kukamilika kwa matengenezo na atakileta katika eneo ambalo kitafanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara kwa upande wa Mlimba na Malinyi, tayari wenzetu wa TARURA walishaambiwa kwa kusaidiana na wenzao wa TANROADS kuhakikisha kwamba, wakati maegesho ya kivuko yanakamilika na pantoni iko pale, kuweza kuwepo barabara za kuwasafirisha wananchi kwa upande wa Malinyi na Mlimba, ahsante.
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa gati katika Mto Mnyela, kuunganisha Halmashauri ya Mlimba kupitia vijiji vya Ngalimila na Ngombi?
Supplementary Question 2
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, natambua Serikali ina mpango wa kujenga Barabara ya Garbabi – Mbulu kwa kiwango cha lami na ninatambua pia mnategemea kumlipa mkandarasi ili afanye hivyo; na kwa kuwa, sasa mvua zinanyesha na mkandarasi hana fedha ya kuchonga barabara hii na haipitiki, je, Serikali ina mpango gani wa kumwambia mkandarasi achonge barabara au TANROADS – Manyara? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge iko na mkandarasi tayari na ameshapatiwa advance payment. Namwelekeza tu Meneja wa Mkoa kwa sababu barabara ikishakuwa na mkandarasi ndiye anayekuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba hiyo barabara inapitika. Kwa hiyo, amsimamie ili huyo mkandarasi aweze kurekebisha njia wananchi waweze kupita, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved