Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y. MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kutafuta soko la asali?
Supplementary Question 1
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha shamba la nyuki la mfano kwa ajili ya ufugaji nyuki?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Serikali ina mpango gani wa kurahisisha upatikanaji wa zana za ufugaji nyuki kama mizinga na nguo za warina asali?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Maige kwa maswali yake ambayo yanalenga kusaidia wananchi katika sekta hii ya asali.
Mheshimiwa Spika, tayari Serikali ilishaanza kufanya kazi za kuwasaidia wafugaji nyuki kupata maeneo ya kufugia nyuki ili kupata asali. Mojawapo ni katika Mashamba ya TFC, kwa maana ya wenzetu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, ambao wana mashamba mengi ikiwepo kule Rufindi, Itigi na maeneo mengine ya Tabora, kule Sikonge, na kadhalika.
Mheshimiwa Spika, yote haya yanalenga kuwasaidia wananchi ili wapate mashamba darasa na maeneo mazuri ya kufugia nyuki ambayo itasaidia kupata asali nzuri. Pia, katika maeneo hayo kuna viwanda vya kukamua asali.
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Katika maeneo hayo pia, kuna taasisi mbalimbali ambazo zinatoa mizinga ya kisasa ambayo inasaidia kuvuna asali nyingi kwa maana ya kufuga kisasa nyuki ambao wanatoa asali ya kutosha ili ziwe na tija kwa wafugaji wa nyuki ambao wamelenga kupata uchumi kupitia kuuza asali, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved