Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, upi uwiano wa madaktari na wagonjwa nchini?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba majibu ya Mheshimiwa Waziri ni sahihi na Wizara hii siyo ya kwake lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa madaktari wengi wako katika ngazi ya degree (shahada ya kwanza) lakini huku chini kwenye vituo vya afya pamoja na zahanati kuna Assistant Medical Officers na Clinical Officers ndio wanaohudumia jamii kubwa ya Watanzania. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba katika hizi ngazi za msingi tunakuwa na Assistant Medical Officers na Clinical Officers wengi zaidi kuliko hao madaktari wa ngazi ya degree?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI K.n.y. WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Shangazi kwa niaba ya muuliza swali Mheshimiwa Husna Sekiboko.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na juhudi za kutoa vibali kwa ajili ya kuajiri madaktari ambao wame-qualify (Degree holders wa Medical Doctors) kwa mwaka juzi iliajiri madaktari 1,200 na mwaka jana 2023/2024 imeweza kuajiri madaktari 1,500. Wakati huo huo Serikali inaendelea kutoa vibali kwa ajili ya kuajiri paramedical pamoja na wale madaktari wa chini (Assistant Medical Officers, Clinical Officers na Assistant Clinical Officers) kwa ajili ya ku-support hii kada ya udaktari kwa kutoa huduma kwa wananchi. Kwa hiyo, ni kwamba Serikali imeendelea kutoa vibali na watumishi wa afya kwa ujumla wanaendelea kuajiriwa; na mwaka huu Serikali imeajiri watumishi zaidi ya 12,000.