Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kiswaga Boniventura Destery

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magu

Primary Question

MHE. KISWAGA B. DESTERY aliuliza:- Pamoja na kwamba polisi ni walinzi wa raia na mali zao, ila wanakabiliwa na changamoto za nyumba za kuishi, maslahi duni na ukosefu wa vitendea kazi:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha vitendea kazi kama magari na mafuta? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za askari polisi na kuboresha mishahara yao?

Supplementary Question 1

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na ninashukuru majibu ya Serikali. Naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza.
(a) Kwa kuwa Serikali imekiri kwamba kuna upungufu wa vitendea kazi, kwa maana ya magari na mafuta; je, ikiongeza kununua magari, italipatia Jeshi la Polisi Wilaya ya Magu hasa Kituo cha Kabila gari lingine?
(b) Kwa kuwa Jeshi la Polisi ni walinzi wa mali na raia lakini maisha yao ni magumu sana, hata wanapostaafu, wanaendelea kuwa na maisha magumu.
Je, Serikali kwa sababu askari katika Wilaya ya Magu wako 135 na nyumba wanazoishi askari kumi ziko tano tu; Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba Wilaya ya Magu? Nipatiwe majibu ni nyumba ngapi zitakazojengwa. (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Magu kuongezewa gari moja, ni kwamba sasa hivi, Kituo cha Magu kina gari tatu tayari, lakini nadhani zitakapokuwa tayari hizi gari nyingine ambazo nimesema kwamba kuna gari jumla 777 zinatarajiwa kukamilika, ukiacha zile ambazo zimeshatolewa, hilo jambo tutalichukua na tutalifanyia kazi. Ni jambo ambalo linawezekana, tutalizingatia.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kuhusiana na nyumba. Kwanza nirekebishe tu, Magu kuna askari 147 siyio 135 kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema. Kwa hiyo, suala la nyumba kama ambavyo nimezungumza kwamba kuna mpango wa kujenga nyumba 4,136 na katika Mikoa ambayo nyumba hizo zitajengwa, Mwanza ni mojawapo. Labda baadaye tuangalie katika orodha ya nyumba zitakazojengwa Mwanza kama Magu ipo. Kama haipo vilevile ni jambo ambalo tunaweza kuliangalia kwa pamoja baadaye.