Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, lini wananchi wa vijiji vya pembezoni mwa barabara ya Lumecha – Londo – Mpepo Morogoro watalipwa fidia?

Supplementary Question 1

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali moja dogo la nyongeza lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni miaka 17 sasa tangu Serikali itwae maeneo ya pembezoni mwa barabara hiyo kwa wananchi na kwamba wananchi bado hawajapewa fidia. Je, Serikali imejipangaje kufanya mapitio upya ya tathmini ili watakapokwenda kulipwa walipwe pesa kulingana na thamani iliyopo sasa?

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Miundombinu bajeti iliyopita alisimama hapa na kusema kwamba barabara hii inakwenda kujengwa kwa mtindo wa EPC+F na kwamba barabara hii haijaanza kujengwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba barabara hii inaanza kujengwa badala ya hizi stori stori wanazotupa sasa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma tunazichoka? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nianze kujibu swali la kwanza la Mheshimiwa Mbunge). Sheria iko wazi ikiishapita miezi sita baada ya kufanya usanifu wananchi hawa wanastahili fidia na kama imepita miaka miwili tunatakiwa tufanye mapitio tena na kutafuta gharama za fidia kwa upya kabisa. Kwa hiyo, kama miaka ni 17 nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ili kuwalipa wananchi hao fidia maana yake zoezi hilo litarudiwa upya ili tuende na gharama ya sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili la Mheshimiwa Mbunge ambalo ni suala la ujenzi tofauti na fidia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba nilishatoa majibu kwamba barabara zote zilizokuwa za EPC+F utaratibu umetengenezwa wa namna ya kuzitekeleza tofauti na mpango uliokuwepo. Kamati ilishaundwa na tayari taratibu zinafanyika ili barabara hii iweze kujengwa kwa utaratibu mwingine tofauti na wa EPC+F. Ahsante. (Makofi)

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, lini wananchi wa vijiji vya pembezoni mwa barabara ya Lumecha – Londo – Mpepo Morogoro watalipwa fidia?

Supplementary Question 2

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri; je, ni lini sasa wananchi waliopisha Barabara ya Uyole - Songwe watalipwa fidia? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni barabara ya Jiji la Mbeya na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama Wizara tulishakamilisha kila kitu na tunategemea muda wowote Wizara ya Fedha kupitia Hazina watatupatia fedha ili wananchi hawa ambao wamepisha huo ujenzi waweze kulipwa fidia zao. Ahsante

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, lini wananchi wa vijiji vya pembezoni mwa barabara ya Lumecha – Londo – Mpepo Morogoro watalipwa fidia?

Supplementary Question 3

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya kutoka Bugene kwenda Itera kuja Songambele kupita Nkwenda, lakini pia kwenda Rwenkorongo, tumeambiwa kwamba ujenzi unaanza na kweli tumeona wakandarasi wameshaanza kujenga maeneo yao ya kukaa kabla ya kuanza, lakini hawa wananchi hawajalipwa fidia kwenye eneo ambako mradi unapita. Nataka kujua, ni lini hawa wananchi watalipwa fidia ili huu mradi uweze kuanza? Nakushukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hakuna mwananchi atakayeondolewa kabla hajalipwa fidia. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba sambamba na kuanza kujenga Serikali pia imeandaa fedha kwa ajili ya kuwalipa kabla hawajavunjiwa mali zao ama nyumba zao. Ahsante.

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, lini wananchi wa vijiji vya pembezoni mwa barabara ya Lumecha – Londo – Mpepo Morogoro watalipwa fidia?

Supplementary Question 4

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa barabara ya Haydom - Mbulu imeanza kujengwa; je, ni lini fidia italipwa kwa wananchi ambao wako katika maeneo ya Barabara ya Haydom - Mbulu?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tathmini ilishakamilika na jedwali lilishapitishwa kwa maana ya uhakiki wote ulishafanyika, tunachosubiri ni kupata fedha ili wananchi hawa waweze kulipwa kabla hatujaanza kuwaondoa. Ahsante. (Makofi)