Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza tozo na kodi za uingizaji wa samaki toka nje ya nchi?
Supplementary Question 1
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa niulize swali moja dogo la nyongeza lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, samaki wana protini nyingi sana, ambapo wajawazito wanatakiwa watumie samaki kwa wingi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba mtoto aliyeko tumboni anaweza kupata virutubisho hivyo pamoja na protini ili akizaliwa aweze kukua vizuri na pia watoto walioko shuleni waweze kutengeneza ubongo wao uwe ubongo wenye ufahamu mzuri.
(a) Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni kwa nini Serikali inachelewesha mchakato huu wa kuhakikisha samaki wanapatikana kwa wingi ikiwemo samaki kuingizwa kutoka nje ya nchi? (Makofi)
(b) Mheshimiwa Naibu Spika, bei ya samaki pamoja na kuwa samaki ni kitoweo muhimu imekuwa ni ghali sana na sasa kula samaki imekuwa ni anasa. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba wanatoa tozo kwenye chakula cha samaki ili kuhakikisha kwamba samaki wanapatikana kwa wingi ikiwa ni pamoja na kununua kwa bei nafuu? Ahsante. (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kabla ya kujibu swali moja la Mheshimiwa Ngonyani lenye sehemu (a) na (b), ninaomba nimpongeze sana kwa ufuatiliaji wa suala hili la samaki na chakula cha samaki.
Mheshimiwa Naibu Spika, siyo kwamba Serikali inachelewesha kufanya tathmini ya tozo mbalimbali. Serikali ipo katika mchakato na wakati huu ni wakati wa maboresho kama nilivyosema katika jibu la msingi. Pendekezo lake Serikali tumelichukua na baadaye tutaleta hapa na Bunge lako Tukufu litapitisha mapendekezo hayo kutoka kwa wadau mbalimbali. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved