Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini ahadi ya Serikali ya kujenga wodi, Kituo cha Afya Kihagara itatekelezwa ili kuondoa changamoto kubwa iliyopo?
Supplementary Question 1
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi na nina maswali mawili. Swali la kwanza; je, ni lini Serikali itajenga wodi na mortuary kwenye Kituo cha Afya Ndalambu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; ni lini Serikali itapeleka vifaa tiba kama X-ray machine, ultra sound pamoja na kujenga majengo yake kwenye Kituo cha Afya Kamsamba?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Mbunge Conchester amefuatilia mara nyingi kuhusiana na ujenzi wa majengo yanayopungua katika Kituo cha Afya cha Ndalambo na ninaomba nimhakikishie tu katika bajeti ya Mwaka ujao wa Fedha 2025/2026 tumeweka mpango, kwa ajili ya kwenda kuongeza majengo katika Kituo cha Afya cha Ndalambo.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusiana na Kituo cha Afya cha Kamsamba, ni kweli, tunafahamu kuna baadhi ya vituo ambavyo vina upungufu wa miundombinu, lakini kuna upungufu wa vifaa tiba ikiwemo X-Ray, Ultra-sound na majengo ya kuhifadhia maiti. Ninaomba nimhakikishie Mbunge kwamba, tunaendelea kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba na majengo hayo kwa awamu na tutahakikisha tunakwenda kuboresha katika eneo hilo la Kituo cha Afya cha Kamsamba. Ahsante.
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini ahadi ya Serikali ya kujenga wodi, Kituo cha Afya Kihagara itatekelezwa ili kuondoa changamoto kubwa iliyopo?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itapeleka Digital X-ray katika Kituo cha Afya Ushetu? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne imepeleka fedha zaidi ya shilingi trilioni moja na bilioni 290 katika vituo vya huduma ya afya msingi kote nchini ili kununua vifaa tiba zikiwemo Digital X-ray. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Dkt. Mnzava kwamba, zoezi hili ni endelevu tutaendelea kutenga fedha, kwa ajili ya vifaa tiba kwa mwaka ujao wa fedha na tutatoa kipaumbele, kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Ushetu. Ahsante.
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini ahadi ya Serikali ya kujenga wodi, Kituo cha Afya Kihagara itatekelezwa ili kuondoa changamoto kubwa iliyopo?
Supplementary Question 3
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini sasa Serikali itatoa fedha za kujenga majengo ya mortuary, Vituka pamoja na Kirakala? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Ninafahamu kwamba, tulitoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na hususan Manispaa, zenye mapato makubwa kama Temeke kuona uwezekano wa kutenga fedha angalau kwa awamu, kwa ajili ya kujenga miundombinu muhimu kama mortuary.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumuelekeza na kumsisitiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kuanza kutenga fedha kwenye mapato ya ndani, kwa ajili ya kuanza ujenzi huo. Pia, Serikali itaendelea kutenga fedha, kwa ajili ya vifaa tiba, kwa maana ya jokofu na vifaa tiba vingine. Ahsante sana.
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini ahadi ya Serikali ya kujenga wodi, Kituo cha Afya Kihagara itatekelezwa ili kuondoa changamoto kubwa iliyopo?
Supplementary Question 4
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Dalai ni moja ya kata ambazo zilitakiwa kujengewa vile vituo vya kimkakati. Nataka kujua ni lini sasa vituo hivyo vitajengwa? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, tumeainisha kata za kimkakati kote nchini ambazo zinakidhi vigezo vya kuwa na vituo vya afya, ikiwemo kata ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja katika Halmashauri ya Chemba. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Monni kwamba, tutahakikisha tunatenga fedha kwenye bajeti zijazo, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo ya kimkakati.
Name
Charles Muguta Kajege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini ahadi ya Serikali ya kujenga wodi, Kituo cha Afya Kihagara itatekelezwa ili kuondoa changamoto kubwa iliyopo?
Supplementary Question 5
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile Kituo cha Afya cha Kisorya kinahudumia wananchi wengi. Je, ni lini Serikali itaongeza wodi katika kituo hicho? Ninakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, tulijenga vituo vya afya kwa awamu ya kwanza majengo matano na tunafahamu kwamba, vituo vingi vya afya vilivyojengwa kikiwemo Kituo cha Afya cha Kisorya vinahitaji ujenzi wa awamu ya pili, kwa maana ya wodi za wanaume, wanawake na watoto. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Kajege pamoja na Waheshimiwa Wabunge wengine wote kwamba, vituo vile ambavyo vimejengwa kwa awamu ya kwanza tutaendelea kuvitengea fedha, kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili ili kukamilisha majengo hayo ya wodi. Ahsante.
Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini ahadi ya Serikali ya kujenga wodi, Kituo cha Afya Kihagara itatekelezwa ili kuondoa changamoto kubwa iliyopo?
Supplementary Question 6
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali iko tayari sasa kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Mwamagembe, ambayo Kituo jirani cha Rungo ni kilometa 70, na kilometa 70 tena, Kituo cha Mitundu? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ikiwa kata hiyo, kwa maana ya umbali inakidhi vigezo na ikiwa kata hiyo inakidhi vigezo, kwa maana ya idadi ya wananchi katika eneo hilo, Serikali itahakikisha inaweka mipango, kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya. Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wafanye tathmini, ili kujiridhisha juu ya vigezo na kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI, mpango kazi wa kuanza ujenzi kwa kutumia mapato ya ndani, lakini na sisi kwa maana ya Serikali Kuu tutaona namna ya kutenga fedha, kwa ajili ya kuanza ujenzi huo ikiwa itakidhi vigezo hivyo. Ahsante.
Name
Cecil David Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini ahadi ya Serikali ya kujenga wodi, Kituo cha Afya Kihagara itatekelezwa ili kuondoa changamoto kubwa iliyopo?
Supplementary Question 7
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, kuna ahadi za viongozi wakubwa, kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Nanganga na sasa hivi tunakaribia kumaliza Mwaka wa Fedha na wewe utakuwa ni shahidi, unakumbuka mwezi wa pili tuliahidiwa kwamba, pesa zote za kujenga vituo vya kimkakati kwenye maeneo mbalimbali zitatolewa. Je, pesa hiyo itatolewa lini kwa sababu mwaka wa fedha sasa unaelekea kwisha?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kwamba, Serikali hii imefanywa kazi kubwa ya ujenzi wa vituo vya afya na Waheshimiwa Wabunge ni mashuhuda wazuri kwamba kazi iliyofanyika ni ya kihistoria katika ujenzi wa vituo vya afya na kazi hii ni endelevu. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutahakikisha tunapeleka fedha, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata hiyo ya Mangaka na nimhakikishie tu kwamba, tunafahamu aliorodhesha kwenye zile kata za kimkakati. Kwa hiyo, ni suala la muda tu tutahakikisha tunapeleka fedha, kwa ajili ya ujenzi huo. Ahsante.