Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha za ujenzi wa kilometa chache za Barabara ya Lupiro, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo na Namtumbo ambayo ni ya Ilani ya CCM?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya kuanza kutenga fedha ya kutengeneza hii barabara kwa sababu imekuwa ya muda mrefu. Hata hivyo, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; je, lini Barabara ya Mahenge – Liwale – Nachingwea mpaka Masasi ambayo ina umuhimu kwa sababu inaunganisha mikoa mitatu ambayo ni Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Lindi na Mkoa wa Mtwara itaanza kujengwa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; swali hili la pili huwa ninaliuliza mara kwa mara humu Bungeni, lakini bado sijapata majibu sawasawa ni kipande cha Kilosa – Mikumi na kipande cha Turiani - Mziha ni lini vitaanza kujengwa ili kusudi kuunganisha Barabara ya kutoka Tanga kwenda mpaka Morogoro na kwenda kwenye Mikoa ya Kusini? Ahsante. (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Mahenge – Liwale - Masasi ni barabara ambayo kwa sasa kimsingi haipo, lakini tulitenga katika mwaka huu wa bajeti na nimelijibu kama siyo jana ni juzi hili swali kwamba sisi kama Wizara tumeshatenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa hiyo Barabara. Nilisema pia ninaendelea kusema kwamba, kwa kuwa ni barabara yote inapita kwenye Mbuga ya Selous kwa maana ya Mwalimu Nyerere tuna wadau wengi ambao tunashirikiana nao ili kufanya usanifu wa barabara hiyo kabla hatujaanza kuijenga. Kwa hiyo, sisi kama Wizara tumeshatenga fedha na taratibu zimeshaanza ya kufanya upembuzi yakinifu na kuona uwezekano wa kuijenga barabara ambayo itaunganisha Mikoa ya Kusini na Morogoro.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye swali lake la pili kuhusu Barabara ya Kilosa - Mikumi. Barabara ya Kilosa - Mikumi itakuwa ndiyo mwendelezo wa barabara ambayo ndiyo iliulizwa kwenye swali la msingi kutokea Songea – Ifakara kuja Mikumi, lakini watu hawa wanapokuja huku wangependa wapitie kuja Kilosa kwa ajili ya kuja Dodoma. Tayari Barabara hii imeshafanyiwa usanifu na tumeshaanza kujenga kwa awamu. Kwa mfano, kutoka Dumila mpaka Kilosa tayari na sasa hivi tunatafuta fedha ya kujenga Kilosa kuja Mikumi ili sasa tuweze kuunganisha Mikumi na Kilosa kwa kiwango cha lami. (Makofi)
Name
Catherine Valentine Magige
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha za ujenzi wa kilometa chache za Barabara ya Lupiro, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo na Namtumbo ambayo ni ya Ilani ya CCM?
Supplementary Question 2
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na ahadi ya muda mrefu ya Serikali ya kujenga kipande cha Barabara ya lami kilometa 10 kutoka Waso kwenda Loliondo Wilaya ya Ngorongoro, Mkoa wa Arusha lakini mpaka sasa ahadi hii haijatekelezwa. Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza ahadi hii kwa wananchi wa Ngorongoro? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli usanifu ulishakamilika na maelekezo yalishatoka kutoka kwa Makamu wa Rais kwamba barabara hiyo ijengwe na tumeshakamilisha taratibu zote. Kwa hiyo, sasa hivi tunatafuta fedha kumlipa mkandarasi malipo ya awali ili kipande hicho cha kilometa kumi kiweze kujengwa. Ahsante.
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha za ujenzi wa kilometa chache za Barabara ya Lupiro, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo na Namtumbo ambayo ni ya Ilani ya CCM?
Supplementary Question 3
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 22 za Barabara ya Isyonje Kikondo?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya kutoka Isyonje kwenda Kikondo aliyoitaja ni barabara ambayo inaunganisha Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Njombe na haiishii Kikondo; kimsingi inakwenda Makete. Katika barabara hii barabara yote yenye kilometa karibu 96.4 imeshafanyiwa usanifu, na tumeshaanza kuijenga kwa kiwango cha lami.
Mhesimiwa Naibu Spika, Serikali tuliamua tujenge eneo ambalo ni korofi (eneo la katikati) ni eneo la Kitulo kwenda Iniho katika ile Mbuga ya Kitulo. Kwa hiyo, tumeshaanza na mkandarasi yuko site. Wakati tunatafuta fedha ya kukamilisha vipande vingine kwa Mkoa wa Mbeya na upande wa kutokea Makete. Ahsante.
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha za ujenzi wa kilometa chache za Barabara ya Lupiro, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo na Namtumbo ambayo ni ya Ilani ya CCM?
Supplementary Question 4
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kolandoto kwenda Mhunze ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu ni barabara ambayo ipo katika mpango wa bajeti ya mwaka huu ambao tunakwenda kuumaliza na katika Bunge liliopita nilipata majibu ya Serikali kwamba barabara hiyo inaenda kutangazwa na kimsingi imo kwenye bajeti hii. Sasa nataka nipate majibu ya Serikali ni lini sasa barabara hii inaenda kutangazwa na kuanza kutekelezwa? Ninakushukuru sana.
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumepanga iko kwenye utaratibu wa kuanza kujengwa hiyo barabara ambayo ni sehemu ya barabara zetu kuu katika nchi yetu. Tunachosubiri sasa hivi ni kuitangaza hiyo barabara kama tulivyokuwa tumeipanga kwenye mpango wa bajeti ya mwaka huu wa fedha.
Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha za ujenzi wa kilometa chache za Barabara ya Lupiro, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo na Namtumbo ambayo ni ya Ilani ya CCM?
Supplementary Question 5
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hii barabara inayotoka Namtumbo kupita Malinyi mpaka Ifakara Serikali imetwambia itajengwa kwa awamu. Je, kwa wakati huu inaweza ikatufungulia kusafirishia wakati inajengwa kwa kiwango cha lami basi angalau tuwe tunapita kuitumia njia hiyo kwa kiwango hicho cha changarawe?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, hii barabara ilikuwa imetangazwa yote. Kwa hiyo, tulitegemea mkandarasi ambaye angekuwepo angeweza kuwa anaifanyia matengenezo. Baada ya kufanya utaratibu tumeshawaagiza Mameneja wa Mikoa ya Ruvuma na Morogoro kuhakikisha kwamba kile kipande ambacho kitajengwa ataendelea na mkandarasi, lakini vipande vilivyobaki ma-regional managers wa-TANROAD wahakikishe kwamba wanazikarabati kupita kipindi chote cha mwaka. Kwa hiyo, kwa kiwango hicho cha changarawe kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge wa Namtumbo.
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha za ujenzi wa kilometa chache za Barabara ya Lupiro, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo na Namtumbo ambayo ni ya Ilani ya CCM?
Supplementary Question 6
MHE. JOSEPHINEN J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itajenga Barabara ya kutoka Kitanga – Kigadye – Helushingo - Nyarugusu mpaka Makere kwa kiwango cha lami?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa barabara hii ya mpakani kati ya Tanzania na Burundi inafanyiwa usanifu, lakini kilichofanyika kwa sasa ni kuunganisha kwanza Wilaya ya Kasulu na Wilaya ya kibondo ambapo Daraja lililokuwa la Malagarasi ndilo linahamishiwa pale na mkandarasi yuko site. Sasa wakati tunajiandaa kutafuta fedha baada ya kukamilisha usanifu kuweza kuijenga kwa kiwango cha lami na hasa tukizingatia hilo eneo ndiko kuna shamba kubwa na kiwanda kikubwa cha miwa, pia ni barabara ya mpakani.