Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza:- Je, lini ATCL itaanzisha usafiri wa Ndege kutoka Dodoma – Mwanza - Mbeya na Arusha ili kupunguza gharama kwa wasafiri wanaokwenda mikoa hiyo?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nishukuru kwa majibu ya Serikali. Hata hivyo, nisikitike tu kwamba majibu haya yamekuwa kila siku yakitia faraja kwamba zitaanza, zitaanza kwa sababu hii ni mara ya tatu nauliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mara ya kwanza walisema wanasubiri ndege ikija. Ikaja ile ndege, lakini hawakubadilisha route, imekuja nyingine hawakubadilisha na leo wanasema mpaka Desemba, 2025.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukumbuke kwamba Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni lango la Miji ya Maziwa Makuu na Makau Makuu sasa hivi Dodoma. Ili kurahisisha pia mawasiliano, hawaoni kama ni usumbufu wa watu kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam halafu wanakuja Dodoma wakati Mwanza pia ni Mji ambao ni wa pili kwa ukuaji wa uchumi na unazalisha sana na abiria wengi wanatoka Kanda ya Ziwa? Swali langu la kwanza; ni lini kwa uhakika usafiri huo utaanza? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; tunayo mashirika mengi ya binafsi ya ndege yakiwemo haya ya AURIC ana ndege ndogo na wanaweza kuwa pia na ndege kubwa; tunayo Coastal line na tunayo pia Precision. Je, Serikali haioni ni muda muafaka sasa wa kuzungumza nao ili waweze kuwa na ndege kubwa zitakazoweza kufanya kazi hiyo kama tulivyoomba, Mwanza – Dodoma, Dodoma - Arusha, Dodoma – Mbeya na mambo mengine kama hayo ili kukuza uchumi wa Taifa hili katika usafiri wa anga? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Mheshimiwa Dkt. Mabula kwa ufuatiliaji wake kwenye upande wa ATCL, lakini nimhakikishie kwamba, Serikali hii imefanya jitihada kubwa sana ya kuongeza au kuboresha usafiri nchini. Sote ni mashahidi, miaka tisa nyuma tulikuwa na ndege moja tu. Serikali imenunua ndege zimefika 16 ikiwemo ndege ya mizigo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mahitaji ni makubwa. Hivi ninavyozungumza hapa, tunaboresha viwanja vya ndege ambavyo havijakamilika karibu nchi nzima. Vitakapokamilika nina uhakika Wabunge wa maeneo hayo nao watakuwa wakisimama hapa wanahitaji ndege. Kwa hiyo, nichukue ushauri wake wa pili alioutoa Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe rai kwa mashirika binafsi yote yanayo-operate, yaliyopo ndani ya nchi yetu pamoja na nje ya nchi yetu ili kutazama fursa ambayo Serikali imewekeza kwenye kujenga miundombinu ya viwanja vya ndege karibu kila mkoa, waone namna gani wanaweza kuleta ndege zao ili kuboresha usafiri, lakini na wao watafanya biashara.
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza:- Je, lini ATCL itaanzisha usafiri wa Ndege kutoka Dodoma – Mwanza - Mbeya na Arusha ili kupunguza gharama kwa wasafiri wanaokwenda mikoa hiyo?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itapeleka usafiri wa ndege kuanzia Dodoma – Tabora mpaka Kigoma? Ahsante. (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inamhakikishia Mheshimiwa Genzabuke na Wabunge wote itapeleka ndege katika maeneo mbalimbali nchini baada ya kukamilisha manunuzi kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved