Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sikudhani Yasini Chikambo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO aliuliza:- Miradi ya Maji ya Benki ya Dunia nchini imekuwa ikisuasua sana na hata ile iliyokamilika maji yamekuwa yakitoka wakati wa mvua tu. Je, ni lini Serikali itakamilisha miradi inayosuasua ikiwemo ile ya Wilaya ya Tunduru?
Supplementary Question 1
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kuchelewa kukamilisha kwa miradi ya maji ya vijiji vya Nandembo, Nalasi, Lukumbule na Amani; je, Serikali haioni kwamba kuchelewa kukamilisha miradi hiyo kutaongeza gharama ya miradi?
Swali la pili, katika majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji amesema vijiji vya Majimaji, Muhesi, Nakapanya na Mchoteka utekelezaji wake haukufanikiwa kutokana na kukosa vyanzo. Je, Serikali ina mkakati gani katika kuhakikisha vyanzo vinapatikana na utekelezaji huu unaanza mara moja kwa sababu jambo hili ni la muda mrefu? Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Isack Aloyce Kamwelwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katavi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza amezungumzia Serikali haioni kwamba kuchelewa utekelezaji wa miradi kuna ongeza gharama; ni kweli ukichelewa utekelezaji wa mradi gharama inaongezeka kwa sababu kuna mabadiliko ya bei ambayo yanatokana na vifaa vya ujenzi, lakini pili wale wakandarasi wanaojenga wameajiri watu wao ile gharama ya mishahara muda unakuwa mrefu, kwa hiyo ni kweli kabisa kwamba kuchelewa kunaongeza gharama ya miradi. Kuchelewa kwa miradi kunatokana na matatizo ambayo yanajitokeza katika mkataba siyo kwamba ni suala ambalo linapangwa na binadamu basi tu ni kwamba, kwa mfano tunachelewa kwa sababu katika utekelezaji wa hii miradi tunasaidiana na wadau ambao ni marafiki zetu ambao wanatusaidia katika utekelezaji wa miradi sasa hela ikichelewa kupatikana basi kwa vyovyote vile lazima mradi uchelewe.
Mheshimiwa Spika, wakati mwingine tuna-design mradi kumetokea mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu vyanzo vinakosa maji kwa vyovyote mradi ule lazima utachelewa.
Swali lake la pili amezungumzia suala la vyanzo, ni kwamba Serikali kwa sasa tayari kwa miradi ambayo haikupata vyanzo study zinaendelea kuhakikisha kwamba miradi hiyo inapata vyanzo na lazima vyanzo vipatikane ili tuweze kukamilisha utekelezaji wa hiyo miradi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved