Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Santiel Eric Kirumba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaunganishia umeme wateja waliolipia kabla ya mabadiliko ya bei katika Halmashauri ya Msalala?
Supplementary Question 1
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Halmashauri ya Msalala imeshatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na Mheshimiwa Mbunge ametoa tofali 1,000 za kuanzia ujenzi. Je, Serikali imejipangaje kukamilisha ujenzi wa ofisi hii? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; ofisi hii ya ki-TANESCO imekuwa na changamoto ya watumishi na vitendea kazi, Serikali imejipangaje kupeleka vitendea kazi pamoja na watumishi? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge yote kwa pamoja kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza Serikali inawapongeza wananchi kwa jitihada hizi walizozifanya za kusaidia katika ujenzi wa ofisi hii na pili, tunashukuru kwa taarifa hiyo, tunaichukua na tutawatuma wataalamu wetu waende kuona kazi ambayo imeanza kufanyika, halafu jambo hili tutaliweka kwenye mipango yetu. (Makofi)
Name
Catherine Valentine Magige
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaunganishia umeme wateja waliolipia kabla ya mabadiliko ya bei katika Halmashauri ya Msalala?
Supplementary Question 2
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru, Wilaya ya Ngorongoro imekuwa na changamoto kubwa ya kukatika katika kwa umeme mara kwa mara. Nimekuwa nikiongea hapa na Serikali imekuwa ikiniahidi kutatua kero hii ambayo ni kubwa sana kwa wananchi wa Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Mheshimiwa Spika, ninataka kufahamu ni lini sasa Serikali itatatua kero hii kubwa?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli katika maeneo kadhaa nchini tuna tatizo la kukatika katika kwa umeme na tatizo hili linatokana na uchakavu wa miundombinu ya kusafirishia umeme. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge waendelee kuwa na subira wakati Serikali inafanya kazi kubwa sana ya kuboresha miundombinu hii. (Makofi)
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaunganishia umeme wateja waliolipia kabla ya mabadiliko ya bei katika Halmashauri ya Msalala?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru, ni kwa nini sasa Serikali isitoe mwongozo wa kuonesha tofauti ya malipo ya kuvuta umeme kwa kiwango cha shilingi 27,000 na shilingi 300,000 kulingana na maeneo? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tayari Serikali imekwisha kutoa mwongozo huo. Tunachoweza kufanya sasa ni kuendelea kutoa elimu ili jambo hili liweze kueleweka kwa upana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved